SEMINA YA WATENDA KAZI WA KANISA 

Miongoni mwa sifa za Uadilifu na za Kidini za Maofisa wa Kanisa ni:

  • Walio na uwezo.
  • Wenye kumcha Mungu.
  • Watu wa kweli wala si wenye ndimi mbili.
  • Wenye kuchukia mapato ya udhalimu.
  • Wenye kujawa Roho wa Mungu.
  • Wenye kujali na kutunza familia zao na mahusiano mema katika familia zao.
  • Wenye kushuhudiwa mema na watu walio nje.
  • Watu wasiolaumika.
  • Wenye kiasi, busara, na hekima.
  • Wenye kujali na kufuata utaratibu
  • Si watu wa kujadiliana (si wenye kuruhusu majadiliano juu ya jambo lililofanyiwa uamuzi).
  • Wasiwe wepesi wa hasira.
  • Wasiwe watu wa kujipendekeza nafsi zao.
  • Walio kielelezo kwa maneno mema na matendo mema, usafi, imani, na upendo.

                   {Kut.18:21; Mdo.6:3; 1Tim.3:1-13; 4:12-16; Tito 1:5-11; 2:1, 7, 8}

 

         

MZEE WA KANISA (Mwangalizi wa Kanisa

Hili ni daraja lenye madaraka makubwa. Mzee wa Kanisa Apaswa awe:

  1. Aliyejitoa kikamilifu kwa Kristo. “Huwezi kuwa na mvuto utakaowabadilisha wengine mpaka moyo wako mwenyewe umenyenyekezwa na kusafishwa na kulainishwa na neema ya Kristo” (Evangelism, uk. 458).
  2. Aliye kielelezo kwa washiriki: Wazee wa kanisa hawana budi kuwa kile wanachotaka wengine kuwa, kuamini kile wanachotarajia washiriki wao kukiamini, na kumpenda Kristo kama wanavyowataka washiriki wao kumpenda. Wazee wanachaguliwa na kuwekewa mikono katika kanisa si kwa ajili ya kufanya kazi ya kanisa tu, bali kudhihirisha tabia ya Kristo.

Kuwa kielelezo sahihi kwa hakika kutajumuisha yafuatayo:

  1. Kuunga mkono mafundisho ya kanisa (Tito 2:1)
  2. Kudumisha mahusiano imara ya familia (1Tim.3:4, 5). Kama mzee wa kanisa, yeye ni sehemu ya familia mbili; familia yake mwenyewe na familia ya kanisa.
  3. Kuwa msafi kingono (Ebr.13:4). Epuka kuvunja miiko ya ngono kwa:

  • Kumpenda mwenzi wako kama nafsi yako.
  • Kuelewa udhaifu wako.
  • Kuwa na tahadhari unapomshauri mtu wa jinsia tofauti.
  • Kuwa imara kiroho. Mit.6:32, 33; Thes.4:3-7 iwe kinga yako.

  1. Epuka ubaguzi wa aina yo yote (Gal.3:28).

  1. Uwe mrudishaji zaka na mtoaji sadaka kielelezo. Ukiwa kielelezo katika hili, unaweza kufanya vingi kuwatia moyo washiriki wa kanisa kuwa mawakili waaminifu.3

Kiongozi wa washiriki:
Karama ya uongozi ni uwezo wa kutoa mwelekeo na mwongozo kwa watu wa Mungu ili watende kazi pamoja kutimiza kile Mungu anachotaka watimize(MwM,49). Soma pia 
Warumi12:8. 

Wapende washiriki wako. Kama ukiwapenda wale unaowaongoza,wengi pia watakupenda. Na kama wanakupenda watafuata uongozi wako.

Unganisha washiriki wako. Wasaidie washiriki kuvuta pamoja kwa umoja. Soma Zab.133:1.

Shauriana na washiriki wako. Lisaidie kanisa lako kupanga malengo yake lenyewe, na pale inapobidi panga na wale unaowaongoza.

Mwezeshaji wa washiriki: Kama mzee, unapaswa uwe mratibu na mwezeshaji ukitumia mvuto wako kumsaidia kila mshiriki wa kanisa lako kukuza uwezo kamili wa karama zao binafsi za kiroho kwa ajili ya ujenzi wa kanisa. Wasaidie washiriki kuzijua karama zao za kiroho, kisha wape mafunzo.

Baadhi ya Majukumu ya Mzee wa Kanisa:

  1. Kulilisha kanisa kupitia mafundisho na mahubiri kanisani na nyumbani mwa washiriki (Mdo.20:28; 1Pet.5:2; Yn.21:15-17).
  2. Kulilinda kanisa kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kanisani.
  3. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote, kupitia idara zote na vyama vyote kanisani.
  4. Kuhimiza uwakili katika nyanja zote::: mwili, wakati,talanta, mali, mvuto,
  5. Kusimamia ibada za kanisa. kuhakikisha kuwa ibada za kanisa (Jumatano, Ijumaa, Sabato); zinaendesha inavyostahili, na wahudumu wanaostahili.
  6. Kuwaandaa wanaotarajiwa kubatizwa. Wale wanaohitaji kujiunga na kanisa wanapaswa kujua kanuni zinazoongoza kanisa hilo; wanapaswa kujua maana ya kutoa maisha yao kwa Kristo.
  7. Kuwashikilia washiriki wapya. Yapo mambo manne uwezayo kufanya:

    1. Wafanye rafiki: Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa wapya. (wajibu wa walezi-MwM, 143)
    2. Wafundishe
    • Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20).
    • Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo.
    • Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.
    • Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato

 

 

  1. 3.   Watembelee:

  • Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho.
  • Waalike nyumbani mwako.

 

  1. 4.   Wahusishe:

  • Washirikishe katika shughuli/programu za kanisa; mfano: huduma za Shule ya Sabato, vijana, uimbaji, kujifunza Biblia, kushuhudia, n.k.
  • Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.

 

  1. Kuwarudisha washiriki waliopotea. Ziko sababu zinazofanya washiriki kupoa kiroho/kurudi nyuma/kupotea; taz. MwM, 136. Ili kuwarejesha; kwanza watambue, kisha watembelee. Hapa ni mashauri saba kuongoza safari yako:

                                                         i.            Uliza maswali kwa busara.

                                                        ii.            Sikiliza kwa makini tena kwa maombi majibu wanayoyatoa.

                                                      iii.            Usilalie upande wo wote katika maongezi yako.

                                                      iv.            Heshimu usiri.

                                                        v.            Waombee.

                                                      vi.            Waalike warejee kanisani.

                                                     vii.            Uwapende.

  1. Kuwatembelea washiriki nyumbani. Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1)       Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2)       Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3)       Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

4)       Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. ….

5)       Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.                                                     – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;                                                                                – mwombee kila mmoja kwa jina lake;                                                                                                                    - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6)       Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7)       Andika.                                                                                                                                                                 - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.                                                                                                                                                    - Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.                                                                                                    - Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini  kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

  1. Kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja. Kiongozi anayejali hushauri na kufariji.    Mwongozo wa kushauri:

                                                         i.            Jifunze kusikiliza kwa makini.

                                                       ii.            Jali ufumbuzi. Usitumie muda mwingi kujadili tatizo, bali jadili zaidi ufumbuzi wa tatizo.

                                                      iii.            Wasaidie wachague mpango.

                                                     iv.            Omba pamoja nao.

                                                       v.            Fahamu wakati unapokupasa kutoa rufaa.

  1. Kuwaunga mkono viongozi wenzake.
  • Mzee, ni mshauri wa idara zote kanisani.
  • Mzee, anapaswa kufahamu mpango wa kila idara.
  • Mzee, apaswa kubuni mbinu za kusaidia idara na vyama kanisani….
  1. Kusimamia vikao vya kanisa (Baraza la Kanisa / Mashauri ya Kanisa), kwa kushauriana na Mchungaji wa Kanisa / Mtaa (Knn, 2005, 8-23, 25).
  2. Kupokea barua na maelekezo toka ngazi za juu za kanisa na kufikisha ujumbe panapohusika.
  3. Kutunza  siri za washiriki na za vikao vya kanisa.
  4. Kupanga/kuratibu huduma maalumu:
  • Ubatizo (MwM, 205-209).
  • Meza ya Bwana (MwM, 217-223) {Sabato ya 12 ya kila robo. Knn, 2005, 8-15}.
  • Kubariki watoto (MwM, 209-214).
  • Uzinduzi wa kiwanja (MwM, 223-226).
  • Kutenga kundi kuwa kanisa.
  • Kuweka wakfu kanisa/jengo (MwM, 214-217).
  • Mazishi (MwM, 229-232).
  • Maombi kwa wagonjwa (MwM, 239-242).
  • Kuweka wakfu nyumba (MwM, 226-229).
  1. Kupanga ratiba ya wahubiri (kwa kushauriana na Mchungaji) na kuisimamia.

 

v  “Mamlaka na Majukumu yao ni mapana mno, lakini hayana budi kutendwa chini ya mwongozo wa mchungaji na mashauriano na baraza la kanisa” (MwM, 43).

 

Mamlaka na kazi ya mzee aliyewekewa mikono yanakomea katika kanisa lile tu alikochaguliwa (Knn, 2005, 7-12; Church Manual, 2010, uk.73).

 

 

v  Kikao cha Baraza la wazee / kikao cha wazee na mchungaji:

  • Chaweza kukutana mara mbili au moja kwa juma….
  • Wajumbe ni maofisa wasimamizi (i.e.:wazee wote, mashemasi wakuu, karani wa kanisa, mhazini, mratibu wa usikivu)….
  • Miongoni mwa mambo muhimu ya kuangalia:

ü  Tathmini ya ibada – lishe, matumizi ya muda, ….

ü  Kuona kwamba kalenda ya matukio inazingatiwa na viongozi wa kila idara na vyama kanisani.

ü  Kuona maeneo ya kushauri utendaji wa idara au chama kanisani.

ü  Kuona kama mkakati wa malezi ya washiriki kwa mafundisho/mahubiri na kutembelea unaenda vyema. Tathmini ifanywe mara moja kila juma.

ü  Kuangalia hali ya fedha ya kanisa kulingana na mahitaji ya kanisa. Kushauri idara ya uwakili na maendeleo kubuni njia za kuongeza warudisha zaka na watoaji kwa mpango kanisani.

ü  Kupitia/kuandaa agenda za kwenda baraza la kanisa/mashauri ya kanisa. Agenda isiyopitia katika kikao hicho, ikitajwa/ikiletwa, ipangwe kujadiliwa kikao kinachofuata. Agenda toka idara huwasilishwa kwa wazee na maelezo.

ü  Kutayarisha ratiba ya wahubiri wa kila robo na kuisimamia.

ü  Kufanya tathmini ya maendeleo ya miradi ya kanisa - uinjilisti, majengo, ….

ü  Kupitia barua toka ngazi za juu za kanisa na kuzifanyia kazi….

Vitabu muhimu kwa mzee wa kanisa:

                                               i.            Biblia – uwe na ratiba ya kuisoma kwa ajili ya kukua kiroho.

                                              ii.            Kanuni za Kanisa – kila sura iwe bayana kwa mzee wa kanisa.

                                            iii.            Mwongozo wa Mzee – kisomwe kila sura na kueleweka.

                                            iv.            Vitabu vya Roho ya Unabii….- kwa kadri ya nafasi/uwezo.

                                             v.            Mwongozo wa kujifunza Biblia (lesson) wa kila robo.

                                            vi.            Kitabu cha Mafundisho ya Biblia – kwa ajili ya darasa la Ubatizo na la Furaha.

                                          vii.            Pastor’s and Elder’s Handbook for Youth Ministry.

 

 

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

                  NJIA 16 ZA KUONGEZA UTOAJI                                                                                                                                                        {Toka Kitabu cha ‘Uwakili na Mtindo wa Maisha TUM’, uk.66-67}

(Mwongozo kwa Wachungaji na Wazee wa kanisa)

  1. Anzisha Kamati ya Uwakili/Fedha ya Mwaka Mzima. Ukuaji wa uwakili ni zaidi ya tukio moja la mwaka. Uwakili ni tendo endelevu linalihitaji mikakati ya kutosha kanisani. Kufundisha kwa vitendo na kuwalisha washiriki mambo ya kiroho ndiyo njia pekee iletayo ufanisi.
  2. Weka malengo makubwa zaidi. Uwezo wa utoaji wa makanisa mengi ni zaidi kuliko unavyoonekana. Malengo makubwa ndiyo yaletayo matokeo makubwa kuliko yaliyotazamiwa.
  3. Rudisha mawasiliano ya Kikristo ya kanisa la awali. Mawasiliano ya makanisa ya awali ya kikristo yalifanywa ana kwa ana, mtu kwa mtu, mkakati katika vikundi vidogo vidogo ndivyo walivyofanikiwa. Lazima tuwatembelee washiriki wote na kuwatia moyo, matokeo yake yatakuwa kama yale ya kanisa la mitume.
  4. Toa zaidi kwa utume. Maofisa wa kanisa(wajumbe wa baraza la kanisa) wawe kielelezo katika utoaji kwa mpango….
  5. Badilisha mtindo wa kumtembelea kila mshiriki. Badala ya kuanza kufuatilia wasioitikia, wafuatilie kwanza unaowatarajia zaidi kuitika. Tumia 85% ya muda wako mahali unapotegemea 85% ya fedha.
  6. Jizatiti. Kuwa mchungaji/mzee wa kanisa unayewezesha wakurugenzi wa uwakili ; usiwafanyie kazi yao. Usizuie juhudi yao. Usikubali kuwa mwenyekiti wa kamati yo yote ya uwakili.
  7. Wapange watoaji wako wazuri. Katika upaliliaji na ukuaji wa uwakili tumia watoaji wako wazuri wakusaidie kuliambukiza kanisa lote kuwa na tabia ya kudumu katika utoaji.
  8. Fundisha umuhimu wa utoaji. Fundisha, hubiri utoaji kwa mpango. Usikingie kifua utoaji wa ahadi ati kwa sababu kanisa linahitaji kupanga mipango yake. Washiriki wanahitaji kufanyia uamuzi juu ya uhusiano wao na Mungu.
  9. Watie moyo washiriki juu ya kutoa kwa mpango. Kutoa zaka na sadaka ni sehemu muhimu ya ibada. Mungu alipanga utoaji wa mpango kwa faida ya mwanadamu ili aokolewe na doa la uchoyo.
  10. Watambue na uwaheshimu watoaji waaminifu. Kwa ruhusa ya watoaji wafahamishe wengine mibaraka wanayoipata kama vyombo vyake.
  11. Eleza jinsi ya kutoa. Kwa familia nyingi, tutoe kiasi gani ni jambo gumu. Jitayarishe kutoa maelekezo na vigezo vitakavyosaidia familia fulani  na siyo maelekezo ya jumla.
  12. Fanya maongezi ya faragha. Ushauri juu y utoaji wa kikristo wapaswa kuwa wa faragha sana na ufanyike nyumbani. Ruhusu jambo hili liwe kati ya mshiriki na mshiriki. Ni vyema wachungaji wasijiingize hapa, mshiriki amsaidie mshiriki. Fikiria mchungaji mwenye washiriki elfu tatu katika mtaa!
  13. Tia moyo utoaji wa ushuhuda binafsi. Njia yenye nguvu na iliyo bora ni ile ya kutoa ushuhuda kwa wale wenye uzoefu wa injili na matokeo ya utoaji mwema.
  14. Waachie wahiriki wajivunie (utoaji). Kadri utoaji unavyopanda kuelekea magoli yake, tangaza habari hizi njema. Endelea kutangaza kadri matoleo yamiminikavyo. Tangaza mafanikio sio ushindwaji.
  15. Waelimishe na mapatie malengo washiriki wapya mara baada ya kubatizwa. Waonyeshe kuwa, kuwa mshiriki wa familia ya Mungu na kutoa ahadi ya ubatizo ni sawa na pande mbili za sarafu moja. Kwamba, kufungamanisha fedha zake na ushirika wa kanisa, hufanya ushirika wake kuwa halisi, bila mashaka.
  16. Fedha za mipango mikubwa zichangishwe tofauti na zingine. “Kama fedha za ujenzi zingelitafutwa kwanza, tena kwa bidii kubwa, kanisa likaonekana halina madeni – Je mambo yangelikuwa vizuri iliyoje?” CS, uk.259, 260.

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

                     VITABU VYA REJEA:                                                                                                     

  • Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.
  • Mwongozo wa Mzee.
  • Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM.

 

 

    KARANI WA KANISA - wadhifa muhimu.

  1. Baadhi ya Majukumu ya Karani wa Kanisa:
    1. Huhudumu kama katibu wa baraza la kanisa.
    2. Huhudumu kama katibu wa mikutano yote ya Mashauri ya Kanisa.
    3. Hutunza orodha sahihi ya washiriki wa kanisa:-
  • Kila jina la mshiriki liwe na kumbukumbu za mapokeo –tarehe ya baraza na jinsi alivyoingia: ikiwa ni kwa ubatizo, kuhamia (barua) au kupokelewa kwa mikono.
  • Kila jina lililoondolewa liwe na kumbukumbu za maondoleo –ikiwa ni kwa barua(kuhama), kuasi, kifo, au kutojulikana aliko.
  1. Hutunza orodha sahihi ya mahudhurio ya Meza ya Bwana:-
  • Orodha ya mahudhurio ya Meza ya Bwana ni sawa na ile ya washiriki wa kanisa (mapokeo).
  • Majina ya wasio washiriki wa kanisa mahalia hawaorodheshwi katika orodha ya washiriki wa kanisa, wala ya mahudhurio ya Meza ya Bwana.
  1. Huandika majina ya wabatizwa katika kitabu cha washiriki mara baada ya ubatizo wao. Kila jina linaloongezwa kwa orodha ya washiriki, liongezwe pia kwa mahudhurio ya Meza ya Bwana.
  2. Kutayarisha na kukabidhi vyeti vya ubatizo, ushirika, kubariki watoto, kwa wahusika kwa wakati.
  3. Kutunza orodha ya mali za kanisa.
  4. Kuandaa taarifa kila robo; a) ya kwenda Konferensi, b) ya kuwasilisha kanisani.
  5. Kutayarisha bajeti ya ofisi yake ya mwaka.
  6. Kutunza siri za washiriki.
  7. Kuzingatia uandishi wa barua za miito:

a)      Ndani ya mtaa;

b)      Nje ya mtaa, ndani ya Konferensi;

c)       Nje ya Konferensi, ndani ya Union au nje ya Union

      Karani wa kanisa huandika barua kwa agizo la Baraza la Kanisa, Mkutano wa Mashauri ya Kanisa, au bodi ya wazee wa kanisa.

  1. Kuratibu zoezi la kuelimisha washiriki juu ya mshiriki na ushirika.

 

  1. Mipaka ya Karani wa Kanisa:
  • Asitunze pembeni orodha ya washiriki waliorudi nyuma au wasiojukana walipo.
  • Asitoe barua kwa mshiriki ye yote aliye chini ya karipio.
  • Asiongeze jina bila idhini ya Kanisa.
  • Asiondoe jina bila idhini ya Kanisa, isipokuwa kwa kifo.

 

                                 REJEA: KANUNI ZA KANISA, Toleo la 17, 2005.

 

 

 

      SHEMASI (m.y. mtumishi wa kanisa) {Mdo.6:3-6; 1Tim.3:8-13; Rum.16:1,2}

v  Wawe kielelezo katika tabia na mwenendo wa Kikristo (wacha Mungu).

v  Shemasi wa kiume sharti awekewe mikono kabla ya kushika kazi yake.

v  Shemasi mkuu (me & ke) ni wajumbe wa baraza la kanisa.

 

  1. Baadhi ya Majukumu ya Shemasi:
    1. Kusaidia katika Ibada na Mikutano,
  • Kukaribisha wageni na washiriki wanapoingia kanisani.
  • Kuhakikisha kuwa waabudu wamekaa katika mpango mpango stahili.
  • Kuhakikisha kuwa kuna utulivu mahali pa ibada.
  • Zamu ipangwe vizuri na kufuatiliwa na shemasi mkuu.
  1. Kutembelea washiriki nyumbani mwao {malezi}
  • Kufanikisha zoezi hili muhimu sana katika malezi ya washiriki, ni vyema kila shemasi awe na nyumba anazohudumia.
  • Mpango mzuri na utaratibu wa kuwatembelea washiriki uwepo;

v  Utembeleaji wa washiriki nyumbani mwao ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1)       Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2)       Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3)       Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

4)       Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. ….

5)       Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.                                                     – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;                                                                                – mwombee kila mmoja kwa jina lake;                                                                                                                    - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6)       Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7)       Andika.                                                                                                                                                                 - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.                                                                                                                                                    - Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.                                                                                                    - Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini  kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

  • Taarifa ya kutembelea hutumwa Konferensi kupitia katibu wa uwakili.

 

  1. Kutunza mali za kanisa,
  • Kuwe na orodha ya mali za kanisa na kutunzwa mahali stahili.
  • Kufanya ukarabati inapobidi.
  1. Kuangalia usafi wa jengo la kanisa, vifaa vya kanisa, na uwanja wake.
  2. Kuwatunza wagonjwa na maskini (mfuko wa wenye shida uwepo).
  3. Kukusanya zaka na sadaka siku ya ibada, kuzihesabu na kuzirekodi, kisha kumkabidhi mhazini, naye kuwapatia stakabadhi kwa kiasi alichokabidhiwa.
  4. Kutunza siri za washiriki.
  5. Kusaidia katika huduma za kanisa:
  • Ubatizo {ufafanuzi wa kuandaa mahali pa ubatizo na kupokea wabatizwa toka majini}.
  • Kutawadhana miguu {ufafanuzi wa namna ya kuhudumia wakati wa jukumu hili}.
  • Meza ya Bwana {ufafanuzi wa namna ya kuandaa mkate na divai na namna ya kuhudumu}.
  1. Kuendesha huduma ya mazishi (shemasi wa kiume)
  2. Kuhudhuria katika bodi ya mashemasi.
  3. Kuandaa bajeti ya mashemasi ya mwaka.
  4. Wawe mstari wa mbele kuhudhuria ibada za kanisa.
  5. B.      Baadhi ya mipaka ya shemasi:
  • Haruhusiwi kuendesha huduma zo zote zile za kanisa zitendwazo na mchungaji aliyewekewa mikono.
  • Haruhusiwi kusimamia mkutano wa kupokea na kuhamisha washiriki.

 

                                  REJEA:  Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

 

 

 

MHAZINI WA KANISA – Kazi Takatifu.

v  Mhazini anaweza kwa sehemu kubwa kuchangia moyo wa uaminifu katika kurudisha zaka na kukuza roho ya ukarimu miongoni mwa washiriki.

Baadhi ya Majukumu ya Mhazini wa Kanisa:-

  1. Mwangalizi/Mtunzaji wa fedha zote na kanisa:-

a)      Fedha za amana – ziendazo Konferensi.

b)      Fedha za kanisa mahalia.

c)       Fedha za mashirika saidizi ya kanisa mahalia (fedha za idara na vyama kanisani)

  1. Kutuma fedha za amana (Trust Funds) kulingana na ratiba ya Konferensi.
  • Kanisa haliwezi kukopa, kutumia, au kuzuia fedha za amana kwa madhumuni yo yote yale.
  1. Kusimamia matumizi ya fedha za kanisa mahalia na za mashirika saidizi kanisani.
  • Fedha za kanisa mahalia hutumika kwa agizo la baraza la kanisa au mashauri ya kanisa.
  • Fedha za idara na vyama (mashirika saidizi) hutolewa kwa idhini ya mabaraza ya idara/vyama husika.
  • Awe mwangalifu kuona kuwa anapewa stakabadhi kwa malipo yote yaliyofanywa.
  • Taarifa ya marejesho ni muhimu kabla kiongozi wa idara/ofisa hajaomba fedha zingine.
  1. Kutoa risti kwa kila pesa anayopokea.
  2. Kulinda kusudi la pesa
  • Mhazini wa Kanisa au Baraza la Kanisa hawana mamlaka ya kuchepusha fedha zo zote kutoka kwa lengo ambalo kwalo zimetolewa.
  1. Kutayarisha na kutuma taarifa Konferensi kila mwezi.
  2. Kutayarisha na kutoa taarifa kwa Baraza la Kanisa na Mkutano wa Mashauri ya Kanisa kila robo.
  3. Kujaza Jicho la Kanisa kila mwezi.
  4. Kuhesabu na kuandika idadi ya wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango (washiriki na wasio washiriki).
  5. Kuelimisha washiriki uzuri wa kutoa zaka na sadaka kwa njia ya bahasha tena kwa mpango.
  6. Kuelimisha washiriki wanaorudisha zaka na kutoa sadaka zao kwa njia ya hawala au hundi ya posta, mlipwaji awe ni kanisa, badala ya mtu binafsi ye yote yule. Kisha awasilishe pay in slip kwa mhazini ili amkatie risti.
  7. Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi.
  8. Kutayarisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka.
  9. Kuzingatia utaratibu mzuri wa kutuma fedha Konferensi:-
  • Pamoja na kuandika vizuri jina na A/C ya Konferensi kwenye pay in slip;
  • Jina la Kanisa linalotoa taarifa liandikwe pembeni kushoto mwa pay in slip;
  • Kuhakikisha muhuri na sahihi ya ‘teller’ wa benki viko sawa.
  1. Kutunza siri za washiriki.

 

 

REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

                           MRATIBU WA USIKIVU

Ni muhimu kwamba wengi walio na shauku iliyokuzwa kupitia juhudi za utume wa kanisa wahudumiwe mara moja. Kufikia hapo, mratibu wa usikivu ambaye anaweza awe mzee wa kanisa achaguliwe wakati wa uchaguzi wa maofisa wa kanisa. Mtu huyu ni mjumbe wa baraza la kanisa na wa Kamati ya Huduma za Uinjilisti wa Washiriki, naye hutenda kazi moja kwa moja na mchungaji na mwenyekiti wa kamati hiyo. Majukumu yanayohusika na wadhifa ni pamoja na :-

  1. Kutunza orodha sahihi ya wale wote wenye shauku, iliyopokelewa na kanisa kutokana na kila chanzo kama vile Huduma za Jamii (Chama cha Dorkas), Sadaka ya Mavuno, mikutano ya uinjilisti wa hadhara, masomo ya Biblia, uinjilisti wa walei, mawasililiano yatokanayo na kushuhudia, kugawa magazeti, uinjilisti wa Shule ya Sabato, uinjilisti wa vitabu, uinjilisti wa afya na kiasi, radio-televisheni, na vitabu vinavyotolewa na kanisa kwa ajili ya utume.
  2. Kumsaidia mchungaji na mwenyekiti wa Huduma za Uinjilisti wa Washiriki katika kuandikisha na kuorodhesha majina ya washiriki wenye sifa kwa ajili ya huduma ya ufuatiliaji.
  3. Kutoa taarifa kwa baraza la kanisa kila mwezi juu ya idadi ya wasikivu waliopokelewa na idadi ya wale waliofuatiliwa. Pale ambapo mtu aliyefuatiliwa anapokuwa amefundishwa vya kutosha, basi akabidhiwe kwa mchungaji.

 

REJEA: Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005; Sura 7-31, 32.

 

KIONGOZI / MKUU WA KUNDI                                                               

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi (Mkuu) wa Kundi:

  1. Kiongozi wa kiroho kundini (akimsaidia Mzee wa Kanisa)

                    i.            Anapaswa kuwapenda wale anaowaongoza

  • Mwenye huruma
  • Awe na tamaa ya kuwasaidia wakue kiroho
  • Kuwapenda licha ya kasoro zao

                  ii.            Tafuta ushauri wa washiriki kundini na kwa Mzee wa Kanisa

 

  1. Kuwaunga mkono watendakazi wenzake kundini
  • Buni mbinu za kusaidia kila mtendakazi afaulu
  • Washirikishe wanakundi katika mipango ya kundi, na ya Kanisa

 

  1. Kulilisha kundi, mzee wa Kanisa asipokuwepo
  • Awe na uwezo wa kuendesha ibada za Kanisa, kuhubiri na kufundisha
  • Kusimamia huduma ya maombi kundini
  • Kutoa mafundisho na semina kulenga mahitaji ya wanakundi

 

  1. Kuunga mkono / kutetea kanuni za Kanisa na Mafundisho ya Kanisa

 

  1. Kushirikiana na Kanisa na Konferensi
  • Kutekeleza mipango toka Kanisa mahalia na Konferensi
  • Kuwaheshimu viongozi hao na kuwaunga mkono
  • Kuwashauri
  1. Kulilinda kundi kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kundini

 

  1. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote.

 

  1. Kuhimiza uwakili katika njanja zote, mkuu wa kundi ukiwa kielelezo (Lk. 12:42)
  • Matoleo: Zaka na Sadaka i.e. utoaji kwa mpango
  • Matumizi ya muda, ikiwemo utunzaji wa Sabato na kazi siku sita.
  • Matumizi ya talanta/karama
  • Kutunza mwili kama hekalu
  • Mvuto
  1.  Kuwashirikisha vijana wadogo na watoto katika huduma za Kanisa na uinjilisti
  2. Kuwashikiria washiriki wapya. Yapo mambo manne uwezayo kufanya:
    1. Wafanye rafiki.  Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa wapya. (wajibu wa walezi-MwM, 143)
    2. Wafundishe.
  • Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20).
  • Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo.
  • Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.
  • Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato
  1. Watembelee.
  • Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho.
  • Waalike nyumbani mwako.
  1. Wahusishe.
  • Washirikishe katika shughuli/programu za kanisa; mfano: huduma za Shule ya Sabato, vijana, uimbaji, kujifunza Biblia, kushuhudia, n.k.
  • Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.
  1. Kusimamia kikao cha kundi
  2. Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi
  3. Kuhimiza uwasilishaji wa taarifa zitokazo kundini kwenda Kanisa mahalia – Mhazini, Katibu wa Uwakili, Huduma za Washiriki, Shule ya Sabato na wengineo.
  4. Kusimamia na kutetea kalenda ya matukio ya mwaka na mpango wa Kanisa.
  5. Kutembelea waashiriki nyumbani;

Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1)       Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2)       Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3)       Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

4)       Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. ….

5)       Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.                                                     – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao;                                                                                – mwombee kila mmoja kwa jina lake;                                                                                                                    - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6)       Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7)       Andika.                                                                                                                                                                 - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo.                                                                                                                                                    - Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao.                                                                                                    - Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini  kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

  1. Kuliandaa kundi kuwa kanisa.

 

 

 

IDARA KANISANI  (ASASI SAIDIZI KANISANI)

  1. A.    KWA NINI IDARA KANISANI?                                                                                                                        Sababu za Kuwepo Idara Kanisani:
  2. Kugawa majukumu
  3. Kuongoa roho
  4. Kutoa ushauri kwa uongozi wa kanisa
  5. Kushirikiana idara moja na nyingine kutenda kazi za kanisa
  6. Kuinua viwango vya kiroho kanisani

Viwango vya Kiroho Vipasavyo Kuinuliwa na Idara Kupitia Utendaji:

  1. Uaminifu katika kurudisha zaka na sadaka
  2. Ununuzi wa miongozo ya kujifunza Biblia
  3. Usomaji wa miongozo hiyo
  4. Mahudhurio katika ibada za kanisa na mikutano ya kiroho
  5. Usomaji wa Biblia kwa mpango
  6. Usomaji wa vitabu vya Roho ya Unabii
  7. Ushuhudiaji.

 

  1. B.    NJIA ZA KUENDESHA IDARA KANISANI:

1)       Tambua ukubwa wa idara unayoisimamia na changamoto zilizopo.

2)       Mwombe Mungu akuongoze na akuwezeshe kutekeleza jukumu alilokupa.

3)       Uliza mashauri toka kwa watu wengine – mf. Mchungaji, mzee wa kanisa, ….

4)       Uwe na mipango/malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu.

5)       Wahusishe wana idara katika mipango/malengo hadi waone kwamba ni yao wala siyo yako tu.

6)       Peleka mipango na mapendekezo kwenye baraza la kanisa.

7)       Wape wenzako madaraka, yaani, washirikishe wenzako katika kutekeleza majukumu.

8)       Weka watu wanaofaa katika nafasi wanazostahili.

9)       Wafundishe (unaowaongoza) katika lugha yao na kasi yao.

10)   Kagua kazi ulizowapa, himiza ufanisi wa kazi; daima watie moyo.

11)   Chukua taarifa ya kazi kwa wakati, peleka katika ngazi zinazohusika.

12)   Shirikiana na maofisa wenzako.

13)   Toa shukrani kwa kazi njema.

14)   Kamwe usifanye matumizi ya fedha za idara bila kuidhinishwa na idara husika kupitia vikao vyake.

 

v  Kiongozi, uwe kielelezo katika usemi, mwenendo, usafi, uwakili wa muda, uaminifu na uadilifu katika nyanja zote.

       <><><> Tuma taarifa iendayo Konferensi kwa wakati, kulingana na utaratibu uliopewa

 

 

IDARA YA HUDUMA ZA WASHIRIKI

Idara ya Huduma za Washiriki hutoa nyenzo na kuwafunza washiriki wa kanisa kuunganisha juhudi zao pamoja na za wachungaji na maofisa wa kanisa katika hitimisho la kutangaza injili ya wokovu katika Kristo.  Lengo ni kuandikisha kila mshiriki katika utendaji wa dhati wa huduma ya Mungu ya uongoaji roho.

 

  1. A.   Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Hduma za Washiriki:
    1. Kuongoza katika kufunza na kuliongoza kanisa katika huduma ya utendaji wa utume.
    2. Mwenyekiti wa Baraza la Huduma za Washiriki
    3. Kuwasilisha kwa Kanisa, katika hduma ya Sabato ya kila mwezi na mikutano ya mashauri ya kanisa, taarifa kuhusu shughuli kamili za utume wa Kanisa.

 

  1. B.    Baadhi ya majukumu ya Katibu wa Huduma za Uinjilisti:
    1. Kufanya kazi kama Katibu wa Baraza la Huduma za Uinjilisti.
    2. Kutoa taarifa kwa Kanisa juu ya shughuli za Huduma za Uinjilisti wakati wa huduma ya Sabato ya kila mwezi wa Huduma za Uinjilisti na katika mkutano mashauri ya Kanisa.
    3. Kuhusika katika manunuzi yote yanayofanywa na Kanisa katika Duka la Vitabu la Waadventista.
    4. Kulifahamisha Kanisa kuhusu nyenzo zinazopatikana kwa ajili ya matumizi yake.
    5. Kupanga sadaka za mara kwa mara ili kuwezesha Huduma za Uinjilisti kupata vifaa kwa ajili ya washiriki kufanyia kazi ya utume pale ambapo vifaa hivyo havipatikani kupitia bajeti ya Kanisa.  Sadaka ya huduma za Uinjilisti kwa ajili ya kusudi hili inaweza kutolewa katika Sabato ya kwanza ya mwezi.
    6. Kuandaa na kuwasilisha kwa wakati taarifa iendayo konferensi kila robo, hali kadhalika ile iendayo mashauri ya Kanisa.
    7. C.   Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Wanaume Waadventista (AMO):
      1. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama
      2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma
      3. Kuongoza wanachama kutekeleza uafuatayo:-
  • Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magazeti, hospitalini, vituo vya kulea watoto yatima, n.k.
  • Kuhudumia Nyumba za wenye shida, wazee wasiojiweza, wakongwe, (kuratibu ukaarabati au ujenzi wa Nyumba)
  • Huduma kwa wagonjwa walio majumbani
  • Huduma ya uinjilisti magerezani
  • Kutoa ushauri
  • Kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima pale inapohitajika.

 

  1. D.  Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa Chama cha AMO:
    1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao vya chama
    2. Ni mtunzaji wa vifaa vya chama
    3. Kupokea michango ya wanacham na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama.
    4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.

 

 

  1. E.   Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Dorkas:
    1. Kuratibu na kusimamia usaji wa wanachama
    2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma
    3. Kuongoza wanachama kutekeleza yafuatayo:-
  • Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magerezani, hospitalini, vituo vya kulea watoto yatima, n.k.
  • Kuhudumia Nyumba za wenye shida (maskini), wazee wasiojiweza, wakongwe (kwa maombi, mavazi, vyakula, n.k.
  • Huduma kwa wagonjwa walio majumbani (kwa maombi, chakula, madawa, n.k.)
  • Huduma ya uinjilisti magerezani
  • Kutoa ushauri nasaha
  • Kushirikiana na chama cha AMO katika utoaji wa elimu ya watu wazima pale inapohitajika.

 

 

  1. F.    Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa chama cha Dorkas:
    1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao vya chama
    2. Ni mtunzaji wa vifaa vya chama
    3. Kupokea michango ya wanachama na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama
    4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.

 

  1. G.   Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Satelite:
    1. Kuona kwa dishi na vifaa vingine vya Satelite vipo katika hali njema
    2. Kupata vipindi vinavyorishwa kwa satellite vifaavyo Kanisa mfano Hope Channel.
    3. Kuwa na ratiba ya kuonyesha program za satellite zenye mafunzo / masomo yaffayo kwa Kanisa. Yaweza kurekodiwa na kuonyeshwa kwa washiriki kwa ratiba mwafaka, usingoje tu mikutano ya uinjili kwa njia ya satellite.
    4. Pale ambapo Kanisa bado halina satellite, kiongozi huyu ahamasishe na kusimamia ununuzi wa vifaa na matumizi yake, akionyesha faida nono za kuwa na nyezo hii muhimu ya uinjilisti.
    5. Kupanga na kusimamia bajeti ya satellite.

 

H. Baadhi ya majukumu ya Mratibu wa Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu:

  • Kupitia kwa Huduma kwa watu walemavu, Baraza la Huduma za Washiriki la kanisa la palepale litoe uangalifu maalumu kwa washiriki na wengine walio walemavu. Likuze programu ya kushuhudia kwa walemavu; likitoa mapendekezo kwa baraza la kanisa kuhusu hatua zitakazowezekana kuchukuliwa ili kufanya vifaa vya kanisa viweze kupatikana kwa urahisi kwa walemavu; kulisaidia kanisa kutatua matatizo ya usafiri kwa walemavu.
  • Mratibu wa Huduma kwa watu walemavu hutumika kama kiungo kwa asasi zinazotoa huduma kwa watu walemavu kama vile Shirika la Huduma za Kikristo kwa Wasioona na kukuza programu za shirika hilo kanisani.

 

                        REJEA:  Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

 

 

 

 

IDARA YA SHULE YA SABATO

Shule ya Sabato ndiyo mfumo kimsingi wa elimu ya kidini ya Kanisa la Waadventista Wasabato na una makusudi  manne: kujifunza Maandiko Matakatifu, ushirika, kuifikia jamii (kushuhudia), na kukazia utume ulimwenguni.

 

  1. A.     Kazi za Maofisa wa Shule ya Sabato:-

 

  1. 1.        Kiongozi (Mrakibu) wa Shule ya Sabato
  •  Anatazamiwa kufuata maamuzi ya Baraza la Shule ya Sabato kuhusu utendaji wa idara.

 

Baadhi ya majumu yake:

                                 i.            Kusimamia viongozi wote wa Shule ya Sabato na kuwatia moyo kutekeleza majukumu yao kwa furaha na mafanikio.

                                ii.            Kuitisha na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Sabato.

                              iii.            Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Kanisa katika idara ya Shule Sabato.

                              iv.            Kusimamia mkutano wa Walimu wa Shule ya Sabato.

                                v.            Kuwakilisha Shule ya Sabato kwenye Baraza la Kanisa.

                              vi.            Kuona kwamba migawanyo yote inafanywa sawasawa.

                             vii.            Kupanga kutimiza mahitaji ya kila divisheni kwa maofisa, vifaa / zana, na fedha.

                           viii.            Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – uinjilisti kuhamasisha VBS, kufanya Matawi ya Shule ya Sabato, na uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato

                              ix.            Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika kutafuta kurudisha washiriki waliorudi nyuma, kwa kuweka hai rekodi za Shule ya Sabato na kuwatia moyo viongozi na walimu kupanga program mathubuti za kutembelea

                                x.            Kuwasiliana na Karani wa Shule ya Sabato juu ya ukamilifu wa rekodi na usahihi wa taarifa na utumiaji wa hizo taarifa haraka kila robo kwenda kwa Mkurugenzi wa Shule ya Sabato Konferensi kupitia kwa Mchungaji wa Mtaa.

                              xi.            Kuhimiza malengo manne ya Shule ya Sabato

                             xii.            Kusimamia mpangilio na uundishaji katika migawanyo kama ifuatavyo:-

  1. Kupanga na kuratibu mikutano ya walimu wa Shule ya sabato
  2. Kuwahi kila sabato asubuhi kuratibisha shughuli, kujibu maswali, kusaidia kutafuta wa badala pale ambapo waliopangwa kawakufika
  3. Kutoa uongozi na kutia moyo viongozi wa migawanyo
  4. Kuwa kiunganishi cha Kanisa na migawanyo mingine kwa kuhimiza matoleo ya Shule ya Sabato ya 13
  5. Kuhimiza mahudhurio katika darasa la walimu.

 

  1. 2.        Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika

Baadhi ya majukumu yake:

  1. Kutunza orodha ya washiriki wa Shule ya Sabato, anuani na namba zao za simu
  2. Kuhimiza utembeleaji wa washiriki wasiohudhuria vyema Shule ya Sabato
  3. Kusaidia kuhusishwa kwa wabatizwa wapya na wahamiaji katika programu za Shule ya Sabato
  4. Kuhudhuria baraza la Shule ya sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango kwa ajili ya kukuza ushirika.
  5. Kuwa tayari asubuhi ya Shule ya Sabato ……

 

  1. 3.        Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Uinjilisti

Baadhi ya majukumu yake:

  1. Kusimamia uinjilisti wa Shule ya sabato katika jumuiya
  2. Kupanga na viongozi wa migawanyo na walimu kwa ajili ya shughuli za uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato
  3. Kupanga kwa ajili ya siku za Wageni
  4. Kupanga pamoja na viongozi wa migawanyo kwa ajili ya siku za maamuzi
  5. Kupanga na Mkurugenzi wa shule ya Sabato wakati wa likizo (VBS) kwa ajili ya program za VBS.
  6. Kupanga na viongozi wa migawanyo kufungua matawi ya Shule ya Sabato
  7. Kukuza ufuatiliaji kwa ajili ya wageni
  8. Kuhudhuria Baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli za mipango kwa ajili ya uinjilisti kwa jamii.
  9. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …….

 

  1. 4.        Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Utandaaji
  • Watandaaji ni washiriki ambao kwa sababu mbalimbali hawawezi kuhudhuria daima vipindi vya Shule ya Sabato. Wanaweza kuzuiwa na:-
  1. Matatizo ya usafiri
  2. Ugonjwa
  3. Uzee
  4. Hali zisizoepukika nyumbani
  • Kiongozi huyo huchaguliwa wanapokuwepo watandaaji  zaidi ya watatu. Wasipozidi watatu, hutunzwa na Karani wa Shule ya Sabato au Msaidizi.

 

Baadhi ya majukumu yake:

                                 i.            Hufanya kazi chini ya Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika

                                ii.            kuwasiliana na washiriki wasioweza kuhudhuria Shule ya Sabato

                              iii.            kuwasiliana na Mchungaji, Mzee / Wazee wa Kanisa, Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika, na yeyote anayeweza kutoa habari za wale wanaopaswa kuandikishwa katika utandaaji.

                              iv.            Kudumisha mawasiliano na watandaaji kwa kuwatembelea ikiwezekana, au barua au simu.

                                v.            Kuhakikisha watandaaji wanapata miongozo ya kujifunza Biblia, somo la nchi za mbali, bahasha za matoleo, vifaa vingine vya Shule ya Sabato vinavyotakiwa ili wapate Baraka zote za Shule ya Sabato.

                              vi.            Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya kitengo chake

                             vii.            Kutoa taarifa kamili ya watandaaji na matoleo yao kwa Karani wa Shule ya Sabato mwisho wa juma, mwezi na robo.

                           viii.            Kuwa tayari asubuhi ya Sabato ……

 

  1. 5.        Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ukarimu

Baadhi ya majukumu yake:

  1. Kufundisha kutoa semina, na kusimamia mabawabu / wakaribishaji.
  2. Kupanga na viongozi wa migawanyo kuhakikisha kuwa somo la misheni lipo katika programu ya Shule ya Sabato.
  3. Kufanya na walimu kuhakikisha washiriki wapya na wageni wanakaribishwa au kanisani.
  4. Kupanga na kuhimiza programu ya kuwakarimu wageni milo, ama majumbani au kanisani.
  5. Kukuza mpango wa ufuatiliaji kwa wageni wote wanaohudhuria Shule ya Sabato ikijumuisha – kadi, barua, simu na / au kutembelea.
  6. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango kuhusu ukarimu.
  7. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …..

 

  1. 6.        Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Utume Ulimwenguni

Baadhi ya majukumu yake:

  1. Kupanga pamoja na viongozi wa migawanyo kuhakikisha kuwa somo la misheni lipo katika programu ya Shule ya Sabato
  2. Kuratibu programu ya Shule ya Sabato ya 13, kutangaza sadaka ya 13 Sabato moja kabla ili kuwatayarisha watoaji.
  3. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango ya ukuzaji wa utume ulimwenguni.
  4. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …….

 

  1. 7.        Majukumu ya Karani wa Shule ya Sabato:
    1. Kuifahamisha Shule ya Sabato kuhusu maendeleo, mwenendo, mipango, na mafanikio yaliyofikiwa kwa kutoa taarifa wakati wa taratibu za kawaida.
    2. Kugawa na kukusanya makadi ya madarasa, bahasha za sadaka na makadi ya taarifa ya huduma yangu kwa Yesu.
    3. Kukagua makadi, kujazia majina yaliyopungua, kuhesabu na kutunza kumbukumbu za fedha.
    4. Kukabidhi fedha zote za Shule ya Sabato kwa mtunza hazina wa Kanisa
    5. Kupata na kutunza risiti za fedha alizokabidhi mhazini
    6. Kuingiza mapema takwimu zote za wiki katika kitabu cha taarifa cha Shule ya Sabato. Taarifa za washiriki na mahudhurio ziingizwe kwa uangalifu mkubwa.
    7. Kutengeneza taarifa kamili na sahihi ya robo ya Shule ya Sabato kwenye fomu ya taarifa na kutuma kwa wakati Konferensi, kupitia kwa Mchungaji wa mtaa.
    8. Kutoa taarifa fupi kila robo na ya mwaka kwenye kitabu cha majina ya washiriki wa Shule ya Sabato.
    9. Kuhakikisha majina ya wana madarasa wote kwenye kitabu kikuu cha majina ya washiriki wa Shule ya Sabato kila mwaka au makadi ya madarasa kila robo.
    10. Kutunza miniti za vikao vya mabaraza ya Shule ya Sabato.
    11. Kuhifadhi vyema taarifa zote katika faili na kuzikabidhi kwa atakayeingia baada yake.
    12. Kuagiza kupitia kwa katibu wa huduma za Kanisa, vifaa vilivyopitishwa na baraza la Shule ya Sabato.
    13. Kuomba vifaa vinavyotolewa bure toka idara ya Shule ya Sabato ya Konferensi.
    14. Kuona kwamba wasaidizi wanajua na kufanya vyema kazi zao, hasa karani anapokuwa hayupo. Washirikishe wakati upo ili wafanye vyema wakati haupo.

 

  1. 8.        Majukumu ya Makarani wasaidizi wa Shule ya Sabato:
    1. Kuzitenda kazi za karani wakati asipokuwepo.
    2. Kutenda kazi kila sabato chini ya maelekezo ya karani mkuu, katika kuyatimiza majukumu kama vile:-
      1. Kusaidia kugawa na kukusanya vifaa
      2. Kushiriki katika kuwajibika kuvitunza vifaa
      3. Kuhesabu sadaka ya Shule ya Sabato
      4. Kutunza kumbukumbu
      5. Kubeba wajibu wa shughuli maalumu kama atakavyopangiwa na karani.

 

  1. 9.        Wajibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Biblia wakati wa Likizo (VBS Director):

Ni wajibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Biblia wakati wa Likizo kufanya yafuatayo:-

  1. Kuongoza katika kuipangilia Shule ya Biblia wakati wa likizo.
  2. Kuihamasisha Shule ya Biblia wakati wa likizo wakati wa Shule ya Sabato
  3. Kufanya ushirikiano na viongozi wasaidizi, walimu, na wasaidizi wengineo kuwafikia watoto kwa ajili ya Yesu
  4. Kukurugenzi (direct) Shule ya Biblia wakati wa likizo, akitumia vifaa vinavyopatikana. Kama vile, masomo ya Shule ya Sabato ya watoto mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu.
  5. Kupanga utaratibu mzuri wa kufuatilia ili chochote kisipotee.  Hii ni pamoja na kutembelea nyumba za wanafunzi wa VBS, na kuwaalika watoto washiriki katika programu zingine zinazopangwa kuleta roho kwa Yesu, kama vile:
    1. Shule ya Sabato
    2. Matawi ya Shule ya Sabato
    3. Wakati wa hadithi (huripotiwa kama tawi la Shule ya Sabato)
    4. Vyama vya biblia vya ujirani (huripotiwa kama tawi la Shule ya Sabato)
    5. Vyama vya watafuta njia
    6. Vyama vya wavumbuzi
    7. Shule ya Kanisa
    8. Kambi la vijana
    9. Huduma za ibada.

 

  1. B.     SIKU MAALUM:

Ziko siku maalum nne, ambazo programu zake hufadhiliwa na idara ya Shule ya Sabato:

                     i.            Siku za kufanya maamuzi (Decision days)

                    ii.            Sabato za kupandisha daraja (Promotion days)

                  iii.            Sabato za Rale za Shule ya Sabato (Rally Days)

                  iv.            Sabato za Wageni (Community Guest Days)

  • Siku hizi maalumu ni za muhimu sana kwa ajili ya kushughudia na malezi
  • Ipangwe programu fupi, ya kuvutia, na ya kiroho … ili kuwavuta kuhudhuria tena au kujiunga na kanisa.
  • Uchaguzi wa mahubiri, mfundishaji, na kwaya ufanywe kwa uangalifu mkubwa ili kukidhi kusudi la program. Mwaliko wa wahudumu hao ufanwe mapema kwa kadri iwezekanavyo kwa kufuata taratibu zilizopo.

 

        I.            Siku za kufanya maamuzi (Decision days)

  • Wadogo kabisa (division ya Chekechea na Shule ya Msingi), mara mbili kwa mwaka.
  • Watoto wakubwa / vijana wadogo, mara moja kwa mwaka
  • Kusudi ni kuwavuta watoto na vijana wadogo kufanya maamuzi kumfuata Yesu
  • Dakika 20-25 zafaa kwa ajili ya programu wakati wa Shule ya Sabato.

      II.            Sabato za kupandisha daraja (Promotion days)

  • Kila mtoto awe radhi  kupanda daraja (darasa) au la, hakuna kulazimisha
  • Ni vyema wazazi kualikwa kuhudhuria.

 

   III.            Sabato za Rale za Shule ya Sabato (Rally Days)

  • Kusudi: kuwaleta washiriki wasiohudhuria Shule ya Sabato kama wageni maalum siku hiyo.

    IV.            Sabato za Wageni (Community Guest Days)

  • Kusudi:
  1. Kulitambulisha Kanisa la Waadventista wa Sabato kwa jumuia iliyo karibu nalo na
  2. Kuongoa roho
  • Ujumuikaji pamoja, mlo uwepo.

 

JINSI YA KUANDAA SIKU MAALUM (maelezo ya jumla)

Idara ya Shule ya Sabato itayarishe mapema:

  1. Itangaze siku maalum
  2. Washiriki wote wahusishwe kualika
  3. Kutuma kadi za mwaliko kwa washiriki wa zamani walio katika jumuia
  4. Teua kamati ya kufuatilia mwaliko, kwa simu, ana kwa ana, barua, n.k.
  5. Weka bango mbele ya Kanisa
  6. Itangazwe katika matangazo ya Kanisa ya kila juma
  7. Teua kamati ya ukaribishaji
  8. Fanya uchaguzi yakinifu ya watakaoshiriki kuendesha programu
  9. Chagua nyimbo zifaazo kwa tukio. Ikiwezekana zichapishwe, nakala za kutosha zipatikane
  10. Kwaya iandaliwe vyema. Nyimbo za kufaa tukio ziandaliwe
  11. Uwe na zawadi kwa wageni
  12. Wafanye wageni wajisikie wamethaminiwa. Wakaribishwe Sabato inayofuata
  13. Tuma barua za shukrani kwa wale walioleta wageni
  14. Andikisha washiriki wapya wa Shule ya Sabato haraka iwezekanavyo.

 

¨¨Hakikisha kwamba kila mgeni aliyealikwa amepata barua / simu au kufikiwa na mtu katikati ya juma linaloishia siku maalum.

Kuandaa kalenda kwa ajili ya Siku Maalum

 

Siku Maalum

Tarehe

Wahusika

Siku za Kufanya maamuzi

 

 

Siku ya kupandisha daraja

 

 

Sabato za Rale za Shule ya Sabato

 

 

Sabato ya Wageni

 

 

            

 

 

PROGRAMU ZA SHULE YA SABATO

 

Programu za kawaida za Shule ya Sabato zapaswa zitumie muda usiopungua dakika tisini (K–K. 8–9). Sehemu ya kwanza ya Shule ya Sabato yapasa kuanza saa tatu kamili asubuhi. Utaratibu huu utakuwa tofauti katika siku maalum za Shule ya Sabato.

 

  1. A.   Dakika 15 za kwanza (3:00 – 3:15) zitumike kwa kumsifu Mungu kwa nyimbo. Huu ni muda mzuri wa Kanisa lote kuimba.  Nyimbo mpya zifundishwe, zinazoimbwa vibaya zirekebishwe, na za zamani ziimbwe pia, na pawepo mchanganyiko mzuri wa angalau wimbo mmoja wa kwaya au kikundi.

 

  1. B.   Dakika 30 zinazofuata (3:15 – 3:45) zitumike kwa programu zitakzohusisha taarifa za utume ulimwenguni (nchi za mbali), ukuzaji wa vipengele mbalimbali vya Shule ya Sabato, na taarifa za ukuaji na maendeleo Shule ya Sabato. Zingatia mashauri yafuatayo:-
    1. Mkuu wa Shule ya Sabato au mmoja wa wasaidizi wake ndio wanaopaswa kuwa wenyeviti wa programu hii, na wasiuache wajibu huu kwa mshiriki mwingine yeyote, hata kama ni kikundi kimealikwa kuendesha Shule ya Sabato.
    2. Kila mhusika awepo mahali pake kwa wakati.
    3. Kila mhusika awe mwenye mwonekano mzuri.
    4. Tumia lugha tamu iliyo fasaha na ya kuvutia.
    5. Wakaribishaji wajae tabasamu na uangalifu katika kuwakaribisha watu.
    6. Pangilia programu yako, kila mmoja ajue cha kufanya kwa wakati husika.
    7. Uwe mwanana, ruhusu waabuduo kupumzika katika Nyumba ya Mungu kwa kutowatwika malaumu, amri, maagizo mengi, au maswali mengi.
    8. Epuka kutumia vifupisho visivyo rasmi – kama “S/S”, “SDA”, “Lesoni” “Wasabato”, n.k.

 

UKUZAJI: unapaswa kulenga moja ya malengo manne ya Shule ya Sabato ambayo ni

  1. Kujifunza maandiko matakatifu
  2. Ushirika
  3. Kuifikia jamii inayotuzunguka, na
  4. Kukazia utume ulimwenguni

 

Ukuzaji waweza kuwa juu ya yafuatayo:-

  1. Mahudhurio kwenye Shule ya Sabato
  2. Usomaji wa Biblia wenye mafanikio
  3. Kukariri mafungu
  4. Ushuhudiaji kwa majirani zetu
  5. Madarasa ya watu 6 hadi 8
  6. Sabato ya wageni
  7. Sabato za kupandisha darasa
  8. Kuanzisha na kuendesha tawi la Shule ya Sabato
  9. Sabato ya Rale za Shule ya Sabato
  10. Ununuzi na usomaji wa miongozo ya kujifunza Biblia
  11. Siku za kufanya maamuzi
  12. Matangazo ya Shule ya Sabato

¨ Anayepangwa kutoa ukuzaji, aelezwe mada ya kushughulikia.

¨ Huu si muda wa kuhubiri.

 

 

TAARIFA ZA SHULE YA SABATO

 

Hizo ni za muhimu sana ili kuwafahamisha wanaoisikiliza hali halisi ya Shule ya Sabato, na kuwapa nafasi kujipongeza kwa mazuri wanayofanya, na kujipa changamoto kwa maeneo wanayopungua. Karani wa Shule ya Sabato anawajibika kuandaa taarifa za Shule ya Sabato za kila juma.

 

UANDAAJI WA TAARIFA

Yafuatayo ni muhimu kuhusishwa katika taarifa:

  1. Mahudhurio kwenye Shule ya Sabato, yakionesha wageni walioshiriki, washiriki waliowahi na waliochelewa.
  2. Taarifa za ushuhudiaji.
  3. Taarifa za wenye miongozo ya kujifunza Biblia na ambao wameisoma.
  4. Taarifa fupi za darasa la waalimu na idadi ya madarasa ya Shule ya Sabato yaliyoendeshwa.

 

UTOAJI WA TAARIFA

Yafuatayo yazingatiwe:

  1. Kila taarifa ilinganishwe na iliyotangulia na ioneshe kama kuna kukua, kudumaa, au kurudi nyuma.
  2. Tumia mchoro kuonesha picha ya maendeleo
  3. Si lazima kutoa taarifa linganifu kila Sabato, lakini ni lazima iandaliwe kila Sabato. Usipitishe mwezi bila kutoa taarifa linganifu.
  4. Kila mwisho wa robo, taarifa ya robo nzima, ile inayokwenda Fildi / Konferensi, ikijumlisha nyongeza ya mambo yanayohusu Kanisa mahalia, itolewe mbele ya washiriki kwa namna ya kuvutia.

 

  1. C.   Dakika 60 zinazofuata (3:34 – 4:45) zitumike kwenye madara ya Shule ya Sabato.  Kila darasa liwe na watu wasiopungua 6 na wasiozidi 8. Kila darasa liwe na viongozi watatu. Mwalimu, Mratibu na Katibu.

 

Dakika 20 au 25 za kwanza zitumike kwa shughuli za darasa kwa karani kutoa kwa kifupi picha ya maendeleo ya darasa, kuchukua mahudhurio, na kupanga namna ya kutembelea waliokosekana. Na kwa mratibu kuchukua taarifa za ushuhudiaji na kuhimiza ushuhudiaji.

 

Dakika 35 au 40 zitumike kujadili somo la juma hilo.

 

MUHIMU:  Imesisitizwa sana kuwa kila Sabato tuwe na muda usiopungua dakika 30 za kujifunza Biblia kupitia mwongozo wa kujifunza Biblia.

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

 

                    VITABU VYA REJEA:  <> Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

                                                         <> Sabbath School Handbook .

                                                          <> Mwongozo wa Shule ya Sabato-TUM.

 

 

 

 

KAMATI YA UWAKILI NA MAENDELEO

 

  1. A.     WAJUMBE WAKE:
    1. Idadi ya wajumbe inategemea ukubwa wa Kanisa. Katika makanisa madogo pengine kazi za kamati hii hufanywa na baraza la Kanisa moja kwa moja.
    2. Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-
      1. Mwenyekiti wa kamati
      2. Mzee wa Kanisa
      3. Mtunza hazina wa Kanisa
      4. Karani wa Kanisa
      5. Kiongozi wa uwakili (Katibu)
      6. Na wengine watakaoonekana kuhitajika

 

  1. Mwenyekiti wa kamati hii anachaguliwa kama ofisa wa Kanisa kwa kazi hii, naye ni mjuzi hasa wa miongozo ya Kanisa.

 

  1. B.     SIFA ZA WANAKAMATI:
    1. Wawe watu waliojitoa kikamilifu katika kutekeleza wajibu wa Kanisa
    2. Wawe na uzoefu au ujuzi wa kupanga mikakati au shughuli za maendeleo
    3. Wawe tayari kutoa muda wao na nguvu zao nyingi kwa faida ya utumishi wa Kanisa
    4. Wawe watu wenye mvuto mzuri kwa washiriki wenzao
    5. Juu ya yote wawe mawakili waaminifu

 

 

 

 

  1. C.     KAZI ZA KAMATI:
    1. Kubuni njia za kuendeleza familia Kanisa ili izidi kukua katika neema-kiroho, kijamii, kimwili, na kiuchumi.
    2. Itawaelimisha washiriki namna ya kuishi kwa kujitosheleza kiuchumi kama familia binafsi nyumbani mwao, na kama Kanisa la Kristo katika ngazi zote.
    3. Itawaelimisha washiriki kujua na kutekeleza wajibu wao kama mawakili wa Mungu na watumishi wa Kristo.
    4. Itawaelimisha washiriki namna ya kuongeza si matoleo ya zaka na sadaka tu, pia kuinua kipato chao ili hali yao ya uchumi iinuke.
    5. Itafanya kazi ya kusimamia mipango yote inayohusu kuingia na kutumia fedha za Kanisa.
    6. Itahamasisha utekelezaji wote wa mipango yote ya maendeleo kanisani – kama ujenzi wa makanisa, ujenzi wa Nyumba za watumishi, upatikanaji wa vifaa vya kufanyia uinjilisti, na program zingine za huduma kwa jamii.
    7. Itabuni mbinu na njia za kuongeza mawakili waaminifu kanisani – watoaji wa zaka na sadaka kwa uaminifu, na wenye moyo wa kujitoa zaidi katika kuendeleza kazi ya Mungu.
    8. Itabuni mbinu na njia za kuongeza mawakili waaminifu kanisani – watoaji wa zaka na sadaka kwa uaminifu, na wenye moyo wa kujitolea zaidi katika kuendeleza kazi ya Mungu.
    9. Itabuni utaratibu wa kutambua vipawa na talanta mbalimbali za washiriki wa Kanisa, na kuviingiza katika utumishi wa injili na maendeleo ya Kanisa.
    10. Itapokea na kufanyia kazi mipango na mikakati mbalimbali ya idara ya uwakili kutoka Fildi au Konferensi na kutoa taarifa juu ya maendeleo ya utekelezaji wake
    11. Itafanya kazi zingine zote ambazo mkutano wa mashauri ya Kanisa utaitaka ifanye.

 

 

 

  1. D.    JINSI YA KUFANYA KAZI ZAKE:

Kamati hii inazo sehemu tatu za utendaji zitakazojulikana kama vikundi vya utekelezaji wa kamati.

 

  1. 1.       KIKUNDI CHA ELIMU:

Kikundi hiki kitashughulikia program zote na majukumu yote yanayodai elimu

  1. Kupendekeza masomo wa ajili ya washiriki mwaka hadi mwaka
  2. Kuendesha na kusimamia utolewaji wa elimu kwa washiriki yenye lengo la kuwakomaza kiakili, kiroho na kimwili

Mwenyekiti:  Karani wa Kanisa

 

  1. 2.      KIKUNDI CHA BAJETI NA FEDHA:

Kikundi hiki kinasimamia program zote zinazohusu fedha – utaratibu wa kuingia na kutoka kwa kufuata sera za Kanisa na kutawala fedha na bajeti

  1. Kuandaa jicho la Kanisa na kuhakikisha kuwa linajazwa na linafanya kazi yake.
  2. Kutoa taarifa kwa mshiriki mmoja juu ya matoleo yake kwa kufuatana na matoleo yake na ujazwaji wa jicho la Kanisa.
  3. Kuhakikisha kuwa washiriki wana bahasha kwa ajili ya matoleo yao na kuwaelimisha juu ya matumizi yake.
  4. Kugawa mifuko kwa washiriki kwa ajili ya zaka ya vitu halisi (mahindi, maharage, n.k.)

Mwenyekiti: Mhazini wa Kanisa.

 

  1. 3.      KIKUNDI CHA MIPANGO:

Program zote za kuhamasisha washiriki na kueleza mipango ya kazi zinazotekelezwa na kikundi hiki, mfano:

  1. Kupendekeza mambo ya kufanyika kwa kuyawekea kipaumbele
  2. Kupendekeza magoli ya utendaji wa mwaka
  3. Kupendekeza kalenda ya kazi za Kanisa ikionyesha tarehe za kuanza na tarehe za kumaliza
  4. Kupendekeza matendo ya kufanywa na Kanisa na gharama zote zitakiwazo kuyakamilisha na mahali pa kuzitoa.
  5. Watatathmini waaminifu katika matoleo na kupendekeza njia za kuboresha uaminifu katika matoleo

Mwenyekiti: Katibu wa Uwakili.

 

  1. E.     UTENDAJI NA UTEKELEZAJI:
    1. Mipango yote na maazimio yote ya kamati yanafikiwa kwa pamoja na hatimaye Kanisa linayapitisha kama maazimio yake. Baada ya hatua hii, hatua za utekelezaji zaweza kuendelea kwa kutumia vikundi husika na program. Yaani, kila kikundi kinaweza kukaa na kutekeleza maazimio yanayokihusu bila kusubiri kamati yote.
    2. Wajumbe wa kamati hii huwa watano au zaidi, itajengwa katika vikundi vya utekelezaji kuzingatia uwezo wa wajumbe.
    3. Kamati yote inakaa pamoja angalau mara moja kwa mwezi, siyo kwa robo.  Vikao vya maendeleo vinakutana kila baada ya muda mfupi.

 

 

 

 

                  IDARA YA UWAKILI NA MAENDELEO

Idara ya Uwakili na maendeleo ilianzishwa ili kutimiza mpango wa utaratibu wa utoaji wa ukarimu wa Mungu popote kwa Kanisa lake.  Kwa kuwa wajibu wa uwakili wa mwanadamu wahusu utawala mzima wa maisha, wazo la uwakili hutia nguvu uangalifu hasa wa matumizi ya hekalu la Mungu, wakati, uwezo, na mali aliyonayo.

 

  1. A.     Sifa Za Katibu Wa Uwakili:
    1. Awe kiongozi wa kiroho
    2. Awe ni mtu mwenye mazoea ya kutimiza kanuni za uwakili wa kikristo
    3. Awe anaufahamu mpango wa Kanisa wa mali na wa kiroho
    4. Awe tayari kujitolea kwa wakati wake, kupanga kuinua na kuongoza katika Nyanja alizopewa za wajibu wake akishirikiana na mkurugenzi wa uwakili wa fildi / konferensi, Mchungaji wa mtaa na baraza la Kanisa.
    5. Katibu wa uwakili anafanya kazi kati ya idara ya uwakili ya fildi / konferensi na Kanisa katika kutimiza wajibu wake wa kuelimisha, atatekeleza mpango wa elimu ya kawaida ya idara ya uwakili kama inavyotolewa na kupanuliwa kwa vipindi vyake ili kutimiza haja inayoendelea kuongezeka.
    6. Wajibu huu ni pamoja na kumsaidia mchungaji katika kukazia siku ya uwakili ulimwenguni, kuendesha madarasa ya uwakili, elimu ya zaka na sadaka, na kufundisha njia za msingi ya uwakili wakati wa huduma ya siku ya Sabato au wakati mwingine wowote.

 

  1. B.     Majukumu ya Katibu wa Uwakili Kanisani:
    1. Yeye ni katibu wa kamati ya uwakili kanisani
    2. Husaidiana na mzee wa Kanisa kuandaa taarifa ya uwakili kwenda fildi / konferensi kila mwezi, na kumkabidhi mchungaji wa mtaa kwa tarehe husika.
    3. Kulinda na kulifanyia kazi “Jicho La Kanisa”
    4. Kuandaa taarifa ya mshiriki mmoja mmoja na kumtumia
    5. Kuhamasisha washiriki kurudisha zaka na kutoa sadaka kwa uaminifu huku yeye akiwa kielelezo
    6. Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa baraza la Kanisa mara moja kila robo
    7. Kuhakikisha kwamba kila mipango na mikakati ya kamati ya uwakili ya Kanisa inatekelezwa na wahusika kama ilivyoamriwa na kupitishwa katika kamati ya uwakili ya Kanisa.
    8. Kumsaidia Mchungaji / Mzee wa Kanisa katika kutekeleza mipango mbalimbali ya uwakili toka fildi / konferensi / Union / divisheni.
    9. Kuhakikisha kuwa elimu ya uwakili inatolewa kanisani kwa washiriki wa rika zote na yeye mwenyewe akiwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.
    10. Kutembelea washiriki katika harakati za kukuza elimu ya uwakili katika maisha yao.
    11. Kuhakikisha kuwa kupindi cha somo la matoleo cha kila Sabato kina mhudumu na anafanya kazi yake inavyostahili.
    12. Kutayarisha na kusimamia semina za namna ya kujiajiri.
    13. Kuratibu na kusimamia juma la uwakili kama linavyoonyeshwa katika kalenda ya matukio ya mwaka.
    14. Utunzaji siri wa washiriki, upendo, uaminifu na uadilifu, umakini na uyakinifu, vyapasa kuuzunguka utendaji wa Katibu wa Uwakili na kamati yake.

 

Ujumbe maalum: Wakati watakapoamka na kuweka maombi yao, utajiri wao, na nguvu zao zote na mali zao zote miguuni pa Yesu, kazi ya kueneza ukweli

itashinda” (4T.475).

 

JICHO LA KANISA

Kifaa muhimu kwa ajili ya huduma ya mchungaji / mzee wa Kanisa / mtunza hazina na katibu wa uwakili wa kanisa.

 

A. Mambo ya kuzingatia katika kulijaza na kulifanyia kazi jicho la Kanisa:

TUNAZITANGAZIA KWAMBA Mapato ya mtu ni ya siri. Hivyo, watu wafuatao ndio wanaopaswa kulifanyia kazi jicho la Kanisa:

  1. Viongozi wa Fildi / Konferensi / Union / Mchungaji Wa Mtaa
  2. M(wa)zee wa Kanisa hilo
  3. Mtunza Kanisa wa Kanisa hilo
  4. Katibu wa uwakili wa Kanisa hilo

 

B. Jicho la Kanisa liwe na sehemu kuu tatu:

  1. Orodha ya washiriki walioko kanisani, likianza na maofisa wa Kanisa hilo
  2. Orodha ya wale ambao hawana ushirika kanisani hapo – wamehamia karibuni na hawajaleta ushirika wao
  3. Orodha ya wanafunzi wa darasa la ubatizo.

 

  1. C.     Matumizi ya jicho la kanisa:
    1. Husaidia kujua maendeleo ya kiroho ya washiriki, Tendo la urudishaji wa zaka na sadaka ni moja ya mazoezi muhimu ya kiroho ambayo hudhihirisha uhusiano uliopo kati ya mtoaji na Mungu wake. Utoaji wa uaminifu huashiria kuwepo kwa uhusiano bora wa kiroho kati ya mtoaji na Bwana Mungu. Utoaji wa uaminifu huashiria kuwepo kwa uhusiano bora wa kiroho kati ya mtoaji na Bwana Mungu. Kwa mantiki hiyo, utoaji huwa ni pima joto la kiroho.
    2. Husaidia katika kutoa taarifa ya maendeleo ya washiriki waaminifu kila robo.
    3. Humsaidia mchungaji au mzee wa Kanisa, kujua wadhaifu na kuwasaidia, na kuwajua waaminifu na kuwatia moyo.
    4. Hutumika wakati wa uchaguzi wa maofisa wa Kanisa
    5. Husaidia kujaza kadi za ushirika na zile za ubatizo
    6. Husaidia kutoa taarifa kwa mshiriki mmoja mmoja juu ya matoleo yake kwa muda uliokusudiwa.
    7. Humsaidia mtunza hazina kutoa taarifa za washiriki kila mwezi kwa mchungaji wa mtaa wakati anapopokea taarifa za matokeo
    8. Huweza kutumika katika uchambuzi wa mahesabu, kama nyenzo ya udhibiti wa ndani wa fedha.                                                                                                                                                             REJEA: Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM.

 

 

IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA

  • Lengo kuu: Kuimairisha familia kama kituo cha ufundishaji wa nidhamu.
  • Huduma za familia hulenga watu katika mahusiano. Huhusika na mahitaji ya wale waliooana, wazazi na watoto, mahitaji ya kifamilia kwa waseja na watu wote katika mzunguko huo mpana wa familia.
  • Malezi ya waumini wote kanisani hayawezi kufanikiwa nje ya kaya na familia

 

A. Majukumu ya Kiongozi wa Huduma za Familia na kamati yake:

  1. Kuanisha familia zilizopo (fomu maalum zaweza kutumika).
  2. Kutembelea familia, kujua changamoto zao, na kuomba pamoja nao.
  3. Kutembelea wajane na wagane mara kwa mara kwa sababu ya matatizo ya upweke wao na kiwasaidia kutatua matatizo yao.
  4. Kuombea familia mbalimbali katika maombi yake ya faragha
  5. Kutia moyo kila familia kuimaisha ibada za familia (madhabahu ya nyumbani). Malezi ya familia hayawezi kukamilika kama familia hazijilishi kiroho.
  6. Kuratibu vijana na watoto wa familia ambao hawajajiunga na vyama vinavyosaidia watoto na vijana kiroho, kuwashauri (kwa kushikisha na wazazi) kujiunga na vyama husika.
  7. Kulisaidia Kanisa kuishi kama familia yenye upendo, kwa kushughulikia maafa, misiba, harusi, magonjwa, kati ya jamii ya waumini.
  8. Kuweka ratiba ya kula pamoja kikanisa, kuimba, kutoa visa, kama njia ya kuleta furaha na amani kati ya washiriki. Wanaweza kushirikisha waimbaji na utaratibu huu wafaa mara moja kwa robo.
  9. Idara ina jukumu la kuangalia kuwa kaya na familia hazisumbuliwi na ukabila, au tabaka la utajiri na umaskini.
  10. Idara inahusika vile vile kuzungumzia unyanyasaji unaofanywa na watu katika kaya na familia.
  11. Jukumu lingine la idara ni kufuatilia habari zinazojulikana za waumini, kushughulikia kiroho kwanza kabla ya kukatwa na Kanisa.
  12. Idara vile vile ina jukumu lingine zito la kuangalia baadhi ya mila zinazotaabisha familia na kaya.
  13. Idara iwe na lengo la kutia moyo watu wote kujiunga na huduma zilizomo kanisani. Idara inapswa kuangalia afya ya Kanisa kiroho na kimwili sawa na wazazi wanavyoangalia afya za watoto na familia nyumbani.
  14. Kuandaa mipango / malengo na bajeti ya idara.
  15. Kiongozi wa idara ana wajibu wa kuhudhuria baraza la Kanisa.

 

B. MIPANGO NA MALENGO YA IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA (Baadhi):

  1. Vijana kufundishwa unyumba ipasavyo kabla ya kufunga ndoa.
  2. Kuwasaidia (kuwashauri) vijana kupima Ukimwi kabla ya kuoana.
  3. Kuwaona watu ambao wamerudi nyuma kiroho kwa sababu zinazochangiwa na migogoro katika kaya / familia.
  4. Pawepo na lengo la kuwatembelea wajane na wagane kila robo.
  5. Kuhamasisha washiriki kutoa michango kwa familia zilizo na dhiki.

 

v  Zaidi soma Kanuni, 2005, 9-38, 39)

 

 

 

IDARA YA HUDUMA ZA UCHAPISHAJI

Idara hii imeundwa ili kuratibu na kusaidia kukuza uinjilisti wa vitabu katika Kanisa la palepale chini ya usimamizi wa Baraza la Huduma za Uchapishaji. Inalisaidia kanisa la pale pale katika ukuzaji mauzo, na usambazaji wa magazeti na vitabu vingine vya utume vinavyouzwa. Idara hutenda kazi na mchungaji, na idara za kanisa katika kupanga njia za hatua kwa hatua za kuwashirikisha washiriki wa kanisa katika kuyatimiza malengo hayo.

 

“Ziko sehemu nyingi ambako sauti ya mchungaji haiwezi kusikika, sehemu zinazoweza kufikiwa kwa machapisho yetu tu-vitabu, vipeperushi na vijizuu vilivyojazwa na kweli za Biblia ambazo watu wanazihitaji” (Colporteur Ministry, p.4)

 

Baadhi ya majukumu ya Mratibu wa Huduma za Uchapishaji wa kanisa:

  1. Kuandaa wainjilisti wa vitabu (kwa kuhamasisha na kutoa mafunzo). Idara inahusika katika kutoa semina za uinjilisti wa vitabu ili kuandaa watu watakaojitoa kwa kazi hiyo. Kupitia Kamati ya Huduma za Uchapishaji, Idara hupendekeza washiriki wa Kanisa wenye vipawa kutenda kazi ya uinjilisti wa vitabu. Ni jukumu la idara kuhamasisha washiriki wakiunge katika kazi ya uinjilisti wa vitabu.

 

  1. Kuweka kiwango na kuisimamia kazi ya kusambaza vitabu na magazeti. Kazi ya kusambaza machapisho yetu ni kazi ya kila mshiriki.

 

  1. Kuumba shauku kubwa miongoni mwa washiriki wa Kanisa kujipatia, kusoma na kuvithamini vitabu vya Ki-adventista vilivyothibitishwa na viatabu vya roho ya unabii ambayo huliainisha Kanisa la Waadventista wa Sabato kama la unabii wa wakati wa mwisho.

 

  1. Kuanzisha mafunzo ya uinjilisti kwa njia ya vitabu. Hii itasaidia washiriki wa Kanisa kupata ufahamu kimawazo na kithiolojia wa asili na utume wa huduma ya vitabu kama shughuli ya kimishonary ya Kanisa mahalia.

 

  1. Kuendeleza na kutekeleza mikakati ya usambazaji vitabu ya washiriki wa Kanisa wenyewe.

 

  1. Kupanga, kutekeleza, kuratibu na kuhakiki shughuli za huduma ya vitabu.

 

  1. Kushauriana na kushirikiana na baraza la Kanisa kuhusu mipango na shughuli za huduma ya vitabu.

 

  1. Kuandaa mikutano ya huduma za vitabu kwa ajili ya Kanisa mahalia na kupata muwezeshaji kutoka ngazi za juu za Kanisa.

 

  1. Kukuzia ununuaji na usomaji wa vitabu vya roho ya unabii kwa ajili ya malezi na ukuaji binafsi wa kiroho.

 

  1. Kukuzia maktaba za kiadventista nyumbani mwa washiriki wa Kanisa.

 

  1. Kuelimisha kwa kutoa mafunzo, kuongoza na kuelekeza Kanisa kenye uinjilisti ulio hai kwa njia ya vitabu na kaika kufahamu asili yake.

 

  1. Kuandikisha washiriki wa Kanisa katika kazi ya vitabu kupitia kwa timu zilizoundwa au kupitia kazi ya mtu mmoja mmoja.

 

  1. Kuagiza vitabu kulingana na vinavyohitajika kupitia kwa katibu wa huduma za washiriki.

 

  1. Kutoa taarifa za shughuli za huduma ya vitabu kwenye baraza la kanisa na mkutano wa mashauri ya Kanisa.

 

  1. Kuwasilisha taarifa konferensi kupitia kwa Mchungaji wa Mtaa.

 

v  Baraza la Huduma za Uchapishaji-Knn, 2005, 9-61….

 

 

 

 

IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

Idara ya Huduma za Wanawake ipo kwa ajili ya kuunga mkono, kutia moyo, na kutoa changamoto kwa wanawake Waadventista wa Sabato katika mwenendo wao wa kila siku kama wanafunzi wa Yesu Kristo na kama washiriki wa Kanisa la ulimwenguni. Utume wa Huduma za Wanawake kwa maana pana, ni sawasawa na ule wa wakristo wote – ule wa kumwiinua Kristo katika Kanisa na ulimwenguni.

 

A. Malengo – Huduma hii inajaribu:

  1. Kuendeleza ukuaji kiroho na kufanyika kwa moyo mpya miongoni mwa wanawake.
  2. Kusisitiza kwamba wanawake ni wa thamani isiyoweza kukadirika kwa sababu ya kule kuumbwa na kukombolewa kwao, na kuwapatia nyenzo kwa ajili ya utumishi kanisani.
  3. Kuhudumia kwa uchambuzi mpana wa mahitaji ya wanawake kwa mahitaji yote, kuchukulia kwa unyeti wake mitazamo ya tamaduni nyingi na makabila mbalimbali
  4. Kuungana na kushirikiana na idara nyingine maalumu za Kanisa ili kuwezesha huduma kwa wanawake.
  5. Kuwashauri na kuwatia moyo wanawake Waadventista wa Sabato, kwa kuanzisha njia za wao kujihusisha na Kanisa ili wafikie uwezo wa kufaa kwao katika Kristo.
  6. Kutafuta njia na jinsi ya kutoa changamoto kwa kila mwanamke Mwadventista Msabato ili atumie karama zake kuchnangia talanta za wengine kadri wanavyofanya kazi bega kwa bega kuendeleza utume wa Kanisa kwa dunia yote.

 

 

 

B. Sifa Za Kiongozi Wa Huduma Za Wanawake

Mwanamke aliye mwepesi wa kuhisi, anayejali, anayejisikia kuwa na mzigo wa huduma na matatizo ya wanawake. Awezaye kuwatia moyo wanawake wengine waendeleze karama zao za kiroho. Awe anaayeweza kufanya kazi vizuri na wanawake kanisani, mchungaji, na baraza la Kanisa.

 

C. Baadhi Ya Majukumu Ya Kiongozi Wa Huduma Za Wanawake

  1. Yeye hutumika kama mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Wanawake
  2. Huhimiza mawazo na mipango ambayo hutumia kwa kiwango cha juu michango ya wanawake kwa utume wa Kanisa.
  3. Kuona kwamba malengo ya idara, kama yalivyoanishwa hapo juu, yanatekelezwa.

 

  1. Kamati Ya Huduma Za Wanawake Na Majukumu Yake – Kanuni Ya Kanisa, Sura 9-41, 59.

 


MUUNDO WA IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE (SDA)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

USOMAJI BIBLIA

Kiongozi / Msaidizi

 

Mafunzo ya pekee

Utunzaji Watoto

Maburudisho

 

Usafi

UTIAJI MOYO

Kiongozi / Msaidizi

 

Uanzishaji wa Mafunzo ya uongozi

Maombi (Vikundi)

Kutembelea kwa kutia moyo

 

Retreat

UINJILISTI

Kiongozi / Msaidizi

 

Kutembelea kwa kusudi la injili

Kusalimia watu siku ya Jumapili

Siku moja kwa mwezi

Kina mama kutoka

Kutembelea kwa kujifunza

Matukio ya kipekee kimsimu

HUDUMA

Kiongozi / Msaidizi

 

Huduma Shule ya awali

Ukarimu

Milo kwa wagonjwa

Kuwaogesha wagonjwa

 

Kupamba maeneo mbali

MISHENI

Kiongozi / Msaidizi

 

Elimu ya Kimisionari

Bodi ya Vitini

Uandishi Vipeperushi / vitabu

Umishonari kwa vitendo

 

 

IDARA YA MIRATHI NA WOSIA (Ezekieli 3:16-21)

 

  1. I.         UTANGULIZI:

Idara ya huduma ya mirathi na wosia ni idara pacha na idara ya uwakili na maendeleo, ina lengo la kuwakumbusha washiriki ukweli kuwa Bwana Mungu ndiye mmilikaji wa mali zote walizonazo na kwamba wanawajibika kwa Mungu wakiwa hai au wakiwa wamekufa. Muhimu zaidi wanapaswa kuandika wosia wa jinsi mali zao zitakavyotumika baada ya kifo kwa ndugu na jamaa zao lakini bila kusahau kazi ya Mungu ambaye ndiye mruzuku na mfadhili mkuu wa uhai na mali zao zote.

 

  1. II.      KWA NINI KANISA LAKO LINAHITAJI MAFUNDISHO YAHUSUYO HUDUMA ZA MIRATHI
    1. Wosia unaokoa fedha. Inagharimu zaidi kufa bila wosia. Wataalam wa mambo ya mirathi wanasema kufa bila kuandaa wosia kiufundi hugharimu mara tano zaidi.

 

Wosia ulioandikwa vizuri unawezesha washiriki kuepuka migogoro chuki na mivutano. Wakati mtu anapokufa bila kuandika wosia huwaachia watu wa nyumbani kwake taabu na fadhaa na kusababisha chuki na mivutano – hata kwa wale ambao ni wakristo. Mungu ametoa ushauri wa maana kwa watu wake kuhusu swala hili nyeti la wosia, ni usalama na busara kuufuata.

 

Mamilioni ya shilingi ambazo zingefanya kazi ya Mungu hupotea kwa sababu ya kushindwa kuelimisha watu wa Mungu kuhusu umuhimu fani hii ya uwakili na hekima ya kupanga matumizi ya baadaye. Washiriki huridhika na kuwa na amani wanapojua kuwa talanta zao zimewekwa wakfu kwa Mungu wao.

 

Tusipojali jambo hili kubwa tutawajibika mbele za Mungu. Wazazi wanatenda dhambi kwa Mungu wanapogawa mali zao kwa watoto wao wasioamini wenye mali za dunia hii madai ya Mungu hayapaswi kupuuzwa. soma 3T. 121.

 

  1. III.   HUDUMA YA MIRATHI NA WOSIA MAKANISANI

 

  1. Kila Kanisa liwe na kiongozi wa huduma za mirathi na wosia. Kama lilivyopendekezwa na kamati ya utendaji wa Tanzania Union – Katibu wa uwakili wa Kanisa achukue jukumu hili hadi maelekezo mengine yatakapotolewa au kama itakavyokuwa imeoneshwa katika kanuni ya Kanisa.
  2. Majukumu ya kiongozi wa idara ya mirathi na wosia kanisani:
    1. Kutoa mada na mafundisho ya mirathi na wosia kwa washiriki.
    2. Kupokea masoma na miongozo ya mirathi na wosia kutoka fildi /konferensi na kufanyia kazi.
    3. Kuhamasisha washiriki kuandaa wosia wa kikristo – unaokumbuka jamaa na haja zao lakini bila kusahau kazi ya Bwana Mungu wako.
    4. Kando ya mafundisho na mahubiri atahamasisha idara hii kwa njia zifuatazo:
      1. Kuandika sentensi fupi katika ubao wa Kanisa kama, je umekumbuka kuandika wosia wako?
      2. Kuweka karatasi ndogo ndogo katika bahasha za zaka na sadaka zinazopelekewa washiriki zenye ujumbe kama huu: je kazi ya Mungu ina sehemu katika mgao wa urithi wako?
      3. Kuandaa na kutoa taarifa ya idara mara moja kwa robo.
      4. Kutoa ushauri kwa washiriki juu ya jinsi ya kuandika wosia kikristo unaokubalika kisheria
      5. Kujua sheria za mirathi na jinsi ya kuandaa wosia unaokubalika.

 

Kipengele kinachaofuata kinaonesha sheria za mirathi na taratibu zake.

 

  1. IV.    SHERIA ZA WOSIA

Wosia: Wosia ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonyesha nia yake jinsi mali yake igawanywe baada ya kufa kwake.

Wosia waweza kuwa wa mdomo au wosia wa kuandika

 

Wosia lazima ushuhudiwe na mashahidi maalumu ambao lazima wawepo wakati mmoja.

 

Mashahidi hawa huchaguliwa na mwenye kutoa wosia mwenyewe.

 

Zaidi ya mashahidi maalumu, mkewe (mwenye kutoa wosia) au wakeze waliopo nyumbani lazima washuhudie vile vile.

 

Watu wanaorithi kitu chochote kwa mtoa wosia hawawezi kuhesabiwa kama mashahidi kushuhudia wosia ule isipokuwa mke au wake wa mwenye kutoa wosia.

 

Wosia hauna nguvu ikiwa mwenye kutoa wosia amepungukiwa akili kwa sababu ya wazimu, ugonjwa, ulevi au hasira ya ghafla.

 

Wosia hauwezi kupingwa hivi kwa sababu zozote au na mtu yeyote, isipokuwa na mtu asiyehusika.

 

Kama mwenye kutoa wosia alikuwa na akili ya kutosha itategemea ushahidi wa wale mashahidi maalumu na wa mke au wake zake, na hata ushahidi mwingine kama upo.

 

Kama mashahidi hawapatani, itakuwa juu ya baraza kupima na kukubali ushahidi.

 

WOSIA WA MDOMO

Wosia wa mdomo na mashahidi wasiopungua wanne – yaani, watu wa ukoo wasiopungua wawili na watu baki wasiopungua wawili.

 

Wosia wa mdomo unaweza kubadilishwa au kufutwa kwa kufuata ule utaratibu ulioelezwa katika vifungu vya 4, 5, na 11.

 

Mashahidi wa wosia wa kwanza ikiwa wapo na waweze kupatikana washuhudie

 

Ikiwa mashahidi wamekufa wote kabla ya mwenye kutoa wosia hajafa, wosia hauwezi kukubaliwa na urithi utagawanyika kufuata mpango wa urithi usio na wosia.

 

Mwenyewe kama anataka kuusia mali yake, lazima atoe wosia mpya.

 

Ikiwa mashahidi wengine wamekufa, lakini walio hai bado hawapungui wawili, wosia utafuatwa.

 

WOSIA WA KUANDIKWA

Wosia wa kuandikwa usiandikwe na kalamu ya risasi, unaweza kupigwa chapa au kuandikwa na wino au na kalamu isiyofutika.

 

Tarehe ya wosia iliyoandikwa lazima iwekwe.

 

Wosia ulioandikwa ushuhudiwe na mashahidi wanaojua kusoma na kuandika yaani mashahidi wasiopungua wawili (mmoja wa ukoo au mmoja mtu baki) – ikiwa mwenyewe hajui kusoma na kuandika.

Mwenyewe atie sahihi yake katika wosia ulioandikwa ikiwa anajua kusoma na kuandika: ikiwa hajui, aweke alama ya kidole chake cha gumba cha kulia.

 

Mashahidi washuhudie sahihi au alama ya mwenye kutoa wosia, na wenyewe watie sahihi zao katika wosia.

 

Karatasi yenye maandiko ya wosia isijazwe wala isiongezwe na mtu yeyote.

 

Wosia ulioandikwa unaweza kubadilishwa au kufutwa kwa kutegemea wosia ulioandikwa mwingine.

 

Wosia ulioandikwa unaweza kuandikishwa au kuwekwa barazani, lakini si lazima ila hiari.

 

Uandikishwaji au wekezaji huu haukubaliwi kuwa uthibitisho wa wosia ikiwa masharti yote ya sheria yaliyotajwa mbele hayakutimizwa.

 

Mtu aliye chini ya umri wa miaka 21 hawezi kutoa wosia ikiwa masharti yote ya sheria yaliyotajwa mbele hayakutimizwa.

 

Wosia ulioandikwa hauwezi kufutwa au kubadilishwa na wosia wa mdomo. Lakini wosia wa mdomo unaweza kubadilishwa au kufutwa na wosia ulioandikwa.

Wakihudhuria mashahidi wote walio hai na wanaoweza kupatikana walioshughulikia wosia wa mdomo.

 

KUHUSU WOSIA ZA AINA MBILI

Mwenye kutoa wosia anaweza kuusia mali yake yote bila kutaja kitu atakachokuwa nacho wakati wa kufa kwake. Ikiwa mwenye kutoa wosia anausia sehemu tu ya mali atakayokuwa nayo, baki itagawanywa kufuata masharti ya urithi usio na wosia isipokuwa kama mtu anayeusiwa angestahili kurithi kufuata mpango wa urithi usio na wosia, mali anayoiachiwa katika wosia itahesabiwa wakati wa kugawanywa baki.

 

Mwenye kutoa wosia ana uwezo kubadilisha mpango wa urithi usio na wosia. Lakini hawawezi kumnyima mrithi kabisa basipo kutoa sababu nzito. Sababu zinazohesabiwa ni nzito za kuwezesha mwenye kutoa wosia kumnyima mrithi urithi wake ni hizi zifuatazo:-

        i.            Ikiwa mrithi amezini na mke wa mwenye kutoa wosia.

      ii.            Ikiwa mrithi amejaribu kumuua, amemshambulia au amemdhuru vibaya mwenye kutoa wosia au mama mzazi wake (yaani, mrithi)

    iii.            Ikiwa mrithi, bila sababu ya haki hakumtunza mwenye kutoa wosia katika shida ya njaa au ya ugonjwa.

 

Ikiwa mrithi ameharibu mali ya mwenye kutoa wosia. Uharibifu wake utahesabiwa katika kukisia sehemu ya urithi atakayostahili kupata.

 

Dini haihesabiwi kama sababu ya kumnyima mtu urithi.

 

Mtu atakayemnyima mrithi urithi wake lazima aseme wazi katika wosia wake na aeleze sababu zake.

 

Mrithi aliyenyimwa urithi wake apate nafasi kujitetea mbele ya mwenye kutoa wosia au mbele ya baraza la ukoo.

 

Mtu ambaye alijua kwamba amenyimwa urithi na ambaye hakushughulika kujitetea, hawezi kupinga wosia baada ya kufa mwenye kutoa wosia. Ikiwa mtu aliyenyimwa urithi hakuwa na habari kabla ya kifo cha mwenye kutoa wosia, atasikilizwa na baraza la ukoo – litakalokuwa na haki ya kukubali au kukataa madai yake.

 

Kama inaonekana kwamba mtu amenyimwa urithi katika wosia posipokuwepo na sababu ya haki, wosia unavunjwa na urithi utagawanyiwa kufuata mpango wa urithi usio na wosia.  Shauri kama hili huamuliwa na baraza la ukoo. Ila mtu anayehusika asiporithika anaweza kufika barazani kwa hakimu.

 

Mume aweza kumwosia mke mazao au mapato ya mali yake mpaka tena aolewe au afe.

 

Kama mume anao wake wengine anaweza kuwausia wote (sio kuwapa wengine na wengine kuwanyima) mazao au mapato ya mali yake kwa kufuata vyeo vya urithi usio na wosia mpaka waolewe tena au wafe.

 

Mjane asiye na watoto anaweza kuusiwa hata mazao au mapato ya ile sehemu ya mali aliyochuma na mume (na ailiyotajwa kifungu 77 ya sheria zinazohusu hali ya watu) ambayo ingalirudi kinyume.

 

Mtu anaweza kumrithisha rafiki yake kitu au vyombo vyake alivyokuwa akivitumia mwenyewe binafsi au sehemu ya urithi isiyozidi fungu la kila mrithi halisi.

 

  1. V.       MAMBO MUHIMU YA KUKUMBUKA UNAPOFANYA WOSIA WA KIKRISTO
    1. Tafuta na jua mapenzi ya Mungu unapofanya wosia.  Ufanye kwa maombi.
    2. Kumbuka kuwa mali zote ulizonazo ni mali ya Mungu Muumbaji wa Mbingu na nchi.
    3. Unapogawa mali zako kumbuka mahitaji ya familia na jamaa yako.
    4. Usigawe mali zako kwa watu wa jamaa au ukoo wako kwa vile ni desturi au mila. Gawa kulingana na kanuni za mapenzi ya Mungu wa mbinguni.
    5. Usisahau kugawa sehemu maalumu kwa ajili ya kazi ya Bwana Mungu wako.
    6. Unapotoa wosia wakati wa kifo si badala ya ukarimu wako wa kawaida ukiwa mzima. Watumishi wa Mungu yawapasa wafanye wosia wao kila siku kwa kazi njema na sadaka za ukarimu kwa Mungu” {Mashauri Juu ya Uwakili, uk.223:3}.
    7. Mara nyingi mali zinazotolewa kwa watoto na wajukuu kwa madhara yao CS. 323.
    8. Wasaidie watoto wako wakati wa uhai wako kuliko kuwapatia mali nyingi wakati wa kifo.
    9. Wosia wa maana ambao wazazi wangeliwapatia watoto wao ni elimu ya kufanya kazi kwa bidii na ukarimu katika maisha yao.
    10. Kile utakachotoa kwa Bwana Yesu ndicho kitakachokuwa chako milele.
    11. Usihofu kuandika wosia. Mpendwa, “Kifo hakitakujia mapema zaidi kwa sababu umeandika wosia wako” {Mashauri Juu ya Uwakili, uk.224:4}.
    12. Hatari ya kumwibia Mungu hata ukiwa kaburini, “watu wengine wanamnyang’anya Mungu mali yake baada ya vifo vyao kwa jinsi wanavyoandika wosia na kuweka mali zao kwa wale wasioamini. Hivyo baada ya wao kumnyang’anya Mungu wakati wa uhai wao.  Humnyang’anya Mungu hata baada ya vifo vyao” 5 T, 155 – 156.
    13. Je hutatoa mali yako mpaka wakati wa kifo? “Wale wanaongoja mpaka wakati wa kifo kabla hawajagawa mali zao, wanazitoa kwa kifo si kwa Mungu” {Mashauri Juu ya uwakili uk.222:3}.

 

  1. VI.    WACHUNGAJI WAWEZA KUSAIDIA WASHIRIKI NA KANISA KWA UJUMLA KWA HABARI ZA WOSIA WA KIKRISTO
    1. Mchungaji anapaswa kuwa na wosia wa kikristo kwa ajili yake nwenyewe (kama mfano mzuri wa kiongozi, kwa washiriki wake), ambao utatunza mali za familia yake kuwapatia kwa ajili ya mahitaji yao na kukumbuka mahitaji ya Mungu.
    2. Kuonyesha daima ubora wa kila mshiriki kuwa na wosia wa kikristo utakaokidhi mahitaji ya familia zao na familia kubwa ya Mungu.
    3. Hubiri mahubiri mawili au zaidi juu ya uwakili katika Kanisa moja kwa robo ukiwa na lengo la kuwaongoza washiriki wako kuwa na uaminifu, uamsho na matengenezo.
    4. Katika mikutano ya mashauri ya Kanisa, mara moja kwa kipindi fulani toa maelezo ya jinsi ambavyo washiriki wanavyoweza kukumbuka Kanisa au pengine shule kwa kutenga asilimia fulani katika wosia wao.
    5. Endesha semina ya wosia na mirathi kanisani. Wasiliana na kiongozi wa idara hiyo katika fildi / konferensi.
    6. Wakati mchungaji anapotembelea washiriki wake anapaswa kujali mambo ya kiroho na bila kusahau yale ya kimwili, anaweza kushauri juu ya usalama wa familia wakati wa baadaye katika swala la wosia wa kikristo. Zaidi ya yote mchungaji awe makini sana asionekane kuwa anamshinikiza mshiriki na kuingilia mambo yake ya binafsi.

 

VII. HITIMISHO:-

Mkazo katika kuhimiza umuhimu wa kuwa na wosia lazima uwe wa kiroho na sio huduma inayolenga kupata fedha.

 

Kuandika wosia ni tendo la imani. Wosia wa kikristo ni chombo kwa ajili ya utukufu wa Mungu na sio kwa utukufu wa mwanadamu. Utoaji wa mali kwa ajili ya Bwana Mungu uwe umejisikia kwa Bwana Yesu Kristo na wala usiwe umesimikwa katika umimi na ubinafsi.

 

Zaidi ya yote ijulikane wazi kuwa kila mtu huacha urithi, wa namna fulani katika maisha yake. Hii ni kwa sababu wakati mtu anapokufa mvuto wake haufi pamoja naye, unaendelea kuzaliana; na mvuto wa mtu mwema, msafi na mtakatifu unaishi baada ya kifo chake kama mwanga wa jua unavyoishia wakati wa jioni – magharibi. Wakati jua linaporusha nuru ya utukufu wake mawinguni, mwanga wake huonekana vilele vya milima muda mrefu baada ya kuzama nyuma ya milima.

Kadhalika kazi ya mtu mwema, msafi na mtakatifu huangaza hata baada ya kukoma kuishi na kutenda. Kazi zao, maneno yao, na mifano yafanane na mwangaza wa mbinguni au kivuli cha giza na kama urithi tunaoutoa utakuwa na baraka au laana kwa wengine. TM. 429.

 

Tumia index to the writings of Ellen G. White. Kupata notes zaidi kuhusu wosia na mirathi.

 

Mwisho: Hebu tumia mwongozo huu mtaani kwako unaposubiri mwongozo wenye maelezo zaidi juu idara hii. Na Bwana wetu Mwema awe msaada wako. Amen

 

REJEA: Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM, uk.18-24.

 

 

MKURUGENZI WA SAUTI YA UNABII (V.O.P.)

 

Baadhi ya Majukumu Ya Mkurugenzi wa Sauti ya Unabii:

  1. Kusimamia uandikishaji wa wanafunzi wa sauti ya unabii. Kanisa zima lihamasishwe kushiriki. Kwa ufanizi zaidi, kuhusisha viongozi wa kila idara na vyama kanisani kuhimiza wana idara na wanachama kujihusisha na uinjilisti kwa njia ya sauti ya unabii.
  2. Kusahihisha masomo akisaidiana na timu ya walimu wa sauti ya unabii, na kumrejeshea mshiriki mwenye mwanafunzi ampelekee masahihisho pamoja na somo jipya.
  3. Kuwatia moyo washiriki wanaoandikisha wanafunzi, kuwahimiza na kuwatia moyo kumaliza kozi.
  4. Kuwatafuta wafadhili wa kununua kozi za masomo ya sauti ya unabii (Promotion kanisani na / au kuwaona watu binafsi) ili shule ya sauti ya unabii ya Kanisa mahalia iwe na kozi za kutosha daima.
  5. Shirikiana na kiongozi wa huduma za uinjilisti kupanga siku za uhamasishaji ili kupata fedha za kununulia masomo na kuhimiza washiriki kuandikisha wanafunzi na kuwaleta
  6. Kuwatia moyo washiriki wapya ambao hawajayasoma, kufanya hivyo.
  7. Kuandaa mahafali na vyeti kwa wahitimu.
  8. Kutunza vyema orodha ya wanafunzi wa sauti ya unabii
  9. Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya kila robo ya kwenda konferensi kupitia kwa mchungaji wa mtaa wakati wa taarifa.
  10. Kutoa taarifa kwa Kanisa kila robo kupitia kwa baraza la Kanisa
  11. Kupokea na kufanyia kazi maelekezo kutoka mkurugenzi wa idara ya sauti ya unabii wa Konferensi.
  12. Kufanyika kazi maelekezo atakayopewa na baraza la Kanisa au mkutano wa mashauri ya Kanisa.

 

  • Shule ya Sauti ya Unabii ni njia nyepesi ya kufikishia watu ujumbe unaookoa. Kila mshiriki atiwe moyo kujihusisha.

 

  • Timu ya wasahihishaji iwe makini ili kuona kila juma masom yamesahihishwa na kurejeshwa kwa wanafunzi. Utaratibu mzuri wa kuchukua masomo na kuwasilishwa kwa masahihisho upangwe na utangazwe.

 

  • Njia zifanywe, kamwe shule isikaukiwe na masomo.

 

 

KATIBU WA MAWASILIANO

  1. A.      Ujuzi na Stadi Zinazotakiwa
    1. Kuzijua vizuri kanuni na taratibu zinazohusika katika nyanja mbalimbali za mawasiliano na mahusiano kama zinavyobainishwa katika kanuni za kanisa.
    2. Awe na uwezo wa kuliwakilisha kanisa kwa usahihi (asiwe mtu aliyeongoka karibuni).
    3. Awe na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
    4. Awe na uwezo wa kubuni na kusimamia mipango ya kazi.
    5. Awe na uwezo wa kaundika kwa namna inayovutia.
    6. Awe na uwezo wa kukutana na watu.
    7. Awe na utayari wa kutenda kazi akipewa.
    8. Ajue njia za kisasa za mawasiliano; kompyuta, kamera, luninga, video, na matumizi ya barua pepe.
    9. B.      Miongoni mwa Majukumu ya Katibu wa Mawasiliano:-
      1. Anatakiwa kuelewa kanisa lake ili kutekeleza majukumu yake ya mawasiliano vizuri.
      2. Atahamasisha utumaji wa taarifa kwa Fild/Konferensi.
      3. Atasaidia/kuwezesha utumaji wa taarifa kwa Konferensi juu ya matukio muhimu kanisani kwa gazeti la kanisa. mfano: parapanda, matukio kama Sabato za wageni, mikutano ya mahubiri, ubatizo, Shule ya Biblia Wakati wa Likizo, n.k.
      4. Ataendesha warsha za mawasiliano, upigaji picha, uandishi, uhariri, n.k. akisaidiana na mkurugenzi wa Konferensi.
      5. Atasimamia program za idara ya mawasiliano kanisani;mfano: programu ya mahubiri kwa njia ya satelaiti.
      6. Awe tayari kupokea na kufanya kazi kutokana na mipango na maelekezo yatakayotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano wa konferensi.
      7. Kutoa taarifa ya kazi kwa baraza la kanisa kila mwezi na mashauri ya kanisa kila robo.
      8. Tuma taarifa ya konferensi mara moja kwa robo.
      9. Atahamasisha uandikishaji wa wanafunzi wa masomo ya Biblia kwa njia ya posta.
      10. Atahamasisha utoaji wa sadaka kwa ajili ya vyombo vya utangazaji wa kanisa na masomo ya Biblia kwa njia ya posta.
      11. Atahakikisha kuwa kanisa lina ubao wa matangazo na unatumika vizuri na kikamilifu.
      12. Atahakikisha kuwa vibao vyenye maelekezo mahali kanisa lilipo vimewekwa sehemu zote muhimu ili kusaidia ye yote anayetafuta kanisa alipate kwa urahisi.
      13. Kumsaidia mchungaji katika maandalizi ya programu mbalimbali na kujihusisha na program kwa njia ya radio na satelaiti, n.k.
      14. C.      Mazingira ya Kazi:-

Yapo mambo kadhaa ambayo ni muhimu kwa ajli ya utendaji kazi mzuri wa Idara ya Mawasiliano katika ngazi ya kanisa mahalia:-

¨       Bajeti ya kuendesha idara

¨       Bajeti ya kutosha ya kusafiri (pale inapolazimu kusafiri)

¨       Miongozo ya kazi ya idara

¨       Kamera ya digital ya picha za kawaida na video

¨       Uongozi mzuri wa kanisa unaowezesha kukua kwa idara

  1. D.     Kamati ya Mawasiliano

Kila kanisa liunde kamati ya mawasiliano, inashauriwa kuwa na wafuatao:-

1)       Katibu wa mawasiliano-mwenyekiti

2)       Mkurugenzi wa Sauti ya Unabii-mjumbe

3)       Mratibu wa satelaiti-mjumbe

4)       Mratibu wa radio-mjumbe

5)       Mratibu wa magazeti-mjumbe

6)       Mwakilishi kutoka vyombo vya habari vya kanisa-mjumbe.

 

 

MRATIBU WA HUDUMA ZA WATOTO

A. Majukumu ya mratibu wa huduma za watoto ni:-

  1. Kuwa mwenyekiti wa huduma za watoto
  2. Kutekeleza mtaala wa Shule ya Sabato na kuwapa mafunzo waalimu na viongozi katika kutumia mtaala huu.
  3. Kupanga na kutekeleza kalenda ya mwaka ya programu za watoto ambazo zitawavuta kwa Kristo na kuwawezesha kushiriki katika shughuli zote za kanisa.
  4. Kuandaa bajeti ya kuwawezesha utekelezaji wa programu zate na shughulu kwa ajili ya watoto.
  5. Kutumika kama wakili kwa ajili ya mambo ya manufaa kwa watoto na mahitaji ya watoto katika: baraza la kanisa; mchungaji; viongozi wa shughuli za watoto {Knn,2005,9-60}.
  6. Kuchukua hatua za maana ili kudumisha kiwango cha juu cha maadili ya tabia kwa watoto kwa kuwachuja viongozi na walimu wa kujitolea.
  7. Kudumisha mawasiliano kwa wazazi na viongozi wa shughuli za watoto, wakiwajulisha juu ya warsha, mikutano maalumu ya watoto, makambi,….
  8. Kutafuta wasaa wa kutumia muda pamoja na watoto ili kudumisha uelewa wa fikra zao na mahitaji yao.
  9. Kwa ubunifu wake aboreshe mazingira ya mikutano ya ibada kwa watoto ili wazidi kujisikia kuwa wao ni sehemu ya familia ya kanisa wakati wa huduma zote za Ibada.
  10. Kusimamia/kuratibu programu za siku ya watoto
  11. Atumike kama chimbuko la Elimu kuhusu huduma za watoto, akifanya kazi sambamba na Mkurugenzi wa Field/Konferensi.

B.   Uhusiano wa idara hii na idara zingine zinazohudumia watoto:-

¨       Idara hii huhudumia watoto wenye miaka 0-14.

¨       Watoto wa umri huu huhudumiwa pia na idara mbili:

                                               i.            Shule ya Sabato ya watoto: miaka 0-15

                                              ii.            Vijana – chama cha Wavumbuzi: miaka 6-9

                                            iii.            Vijana – chama cha Watafuta Njia: miaka 10-15.

¨       Idara hii haichukui majukumu ya Idara ya Shule ya Sabato, au chama cha Watafuta Njia, au Wavumbuzi; badala yake hufuatilia kuona kama vyama hivyo vinawatendea watoto huduma zinazostahili.

¨       Wakati wa Sabato mchana, Idara hii inahusika na watoto wa umri wa miaka 0-5, ambao wanakuwa na mama zao.

¨       Idara hii si sehemu ya Shule ya Sabato.

C.  Kamati ya Huduma za Watoto:

Wajumbe wa kamati hii huchaguliwa kutokana na uwezo wao na moyo wa kupenda na uzoefu wao katika kufanya kazi na watoto. Kwa kawaida wajumbe wake ni viongozi wa Divisheni ya Shule ya Sabato ya watoto, Kiongozi wa Shule ya Biblia Wakati wa Likizo, viongozi wa vijana wadogo, na watu wawili au watatu wanaopenda huduma za watoto.

 

 

                                  IDARA YA VIJANA

  1. A.    Chama cha Vijana Waadventista Wakubwa (AY):

Chama cha Vijana Waadventista ni idara ambayo kupitia kwayo kanisa hutenda kazi kupitia kwa vijana.

Tamko la Utume – Kitovu cha msingi wa huduma ya vijana ni wokovu wa vijana kupitia kwa Yesu Kristo. Tunaelewa huduma ya vijana kuwa ni ile kazi ya kanisa ambayo huendeshwa kwa ajili ya, pamoja, na kupitia kwa vijana.

Jukumu letu ni:

  1. Kuwaongoza vijana kuelewa thamani ya kila mmoja binafsi na kugundua na kuendeleza karama zao za kiroho na uwezo wao.
  2. Kuwapatia nyenzo na kuwawezesha vijana kwa ajili ya maisha ya utumishi pamoja na kanisa la Mungu na jamii.
  3. Kuhakikisha vijana wanaingizwa katika nyanja zote za maisha na uongozi wa kanisa ili kwamba waweze kuwa washirika jamii katika utume wa kanisa.

Malengo makuu ya chama ni:

1)      Kuwafunza vijana kutenda kazi kwa ajili ya vijana wengine,

2)      Kuandikisha vijana wa kulisaidia kanisa lao na “wale wanaodai kuwa watunza Sabato” na

3)      Kufanya kazi “kwa ajli ya wale wasio wa imani yetu.

Katika jitihada za kuyatimiza malengo haya vijana wanahimizwa:

(1). Kuomba pamoja,

(2). Kujifunza Biblia pamoja,

(3). Kushirikiana pamoja katika maburudisho ya Kikristo,

(4). Kutenda kazi pamoja katika vikundi vidogo vidogo vya kushuhudia,

(5). Kukuza busara, ustadi na talanta katika kazi ya Bwana, 

(6). Kuhamasisha ukuaji kiroho.

 

a).  Miongoni mwa Majukumu ya MKURUGENZI WA CHAMA CHA AY:

  1. Kuandaa mikutano ya kawaida na ya mafunzo ya wanachama.
  2. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama.
  3. Kupata kuelewa shughuli za chama kwa makanisa mengine (ya Waadventista wa Sabato) ili kupata mambo ya kutia moyo.
  4. Wape majukumu wengine kama inavyolazimu katika kutekeleza mipango ya chama.
  5. Fahamu majukumu ya kila ofisa wa chama na fanya uwezavyo kuhimiza mafanikio ya chama.
  6. Uwe na ushirikiano wa karibu na mshauri wa chama, na mzee mlezi wa chama.
  7. Kwa kadri inavyowezekana, shirikisha uongozi wa kanisa mipango ya chama mapema. Baada ya kuweka mipango/malengo na kupitishwa na wanachama, iwasilishe kwenye baraza la kanisa.
  8. Watie moyo wanachama kujiunga na kuhitimu Kozi ya Kiongozi Mwadventista na Kiongozi Mkuu.
  9. Kuratibu na kusimamia Matukio ya Shughuli za Vijana kama yalivyoainishwa katika Kanuni za Kanisa(2005,9-22) na miongozo ya chama.
  10. Kuandaa mipango na bajeti ya chama ya mwaka.
  11. Kuhudhuria baraza la kanisa kila linapoitishwa.
  12. Kuwatia moyo wanachama kushiriki mikutano mbalimbali ya chama katika ngazi mbalimbali za kanisa.
  13. Kuwatia moyo wanachama kujali na kushiriki ibada na programu mbalimbali katika kanisa mahalia.
  14. Kusimamia mikutano ya chama ya kila juma, na ya majuma maalumu.
  15. Soma na fahamu vyema mwongozo wa chama ili uifanye kazi kwa uhakika na ufanisi.
  16. Kuwa tayari kuwafikishia wanachama maelekezo toka ngazi za juu za kanisa.
  17. Kusimamia mapendekezo ya watendakazi wengine wa chama ambao hawachaguliwi na kamati ya uchaguzi/baraza la kanisa, na kupeleka kwenye baraza la kanisa kwa ukubali/ushauri.
  18. Kujaza fomu ya taarifa ya idara ya vijana (ya vyama vyote vinne) iendayo Konferensi, na kuiwasilisha kwa wakati.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayogawiwa na mkurugenzi wa chama.

 

b).  Miongoni mwa Majukumu ya KARANI-MHAZINI WA CHAMA CHA AY:

  1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao na mikutano ya chama.
  2. Agawe na kupokea fomu za kujiunga na chama.
  3. Aandike na kutunza orodha ya wanachama.
  4. Atunze kumbukumbu ya mapendekezo/mipango yote ya chama.
  5. Kutunza orodha ya wanafunzi katika vitengo mbalimbali-mfano:wanaosoma Biblia kwa mwaka, wanaojifunza Kozi ya Kiongozi Mwadventista, wanaojifunza Kozi ya Kiongozi Mkuu, n.k.
  6. Kutayarisha taarifa fupi kila robo inayoonesha shughuli za chama zilizofanyika.
  7. Kupokea fedha zote za chama na kuziwasilisha kwa mhazini wa kanisa ili kuzitunza. Fedha hizo zitotolewa kwa mhazini wa kanisa kwa hitaji la chama.
  8. Kutunza kumbukumbu sahihi ya fedha zilizopokelewa na zilizotumika.
  9. Kuagiza vifaa vya chama kwa wakati.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayopewa na mkurugenzi wa chama.

 

c).  Miongoni mwa Majukumu ya MDHAMINI/MSHAURI WA CHAMA CHA AY:

  1. Aelewe malengo, makusudi, na mbinu za programu za chama.
  2. Ni mshauri na mwelekezaji wa viongozi na maofisa wengine wa chama.
  3. Atende kama kiongozi anayewajali vijana; kuelewa mahitaji yao ni muhimu sana ili kutoa ushauri unaofaa kwa wakati ufaao.

 

B. Chama cha Mabalozi:

a).  Miongoni mwa Majukumu ya MKURUGENZI WA CHAMA CHA MABALOZI:

  1. Kuandaa mikutano ya kawaida na ya mafunzo ya wanachama.
  2. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama.
  3. Kupata kuelewa shughuli za chama kwa makanisa mengine (ya Waadventista wa Sabato) ili kupata mambo ya kutia moyo.
  4. Wape majukumu wengine kama inavyolazimu katika kutekeleza mipango ya chama.
  5. Fahamu majukumu ya kila ofisa wa chama na fanya uwezavyo kuhimiza mafanikio ya chama.
  6. Uwe na ushirikiano wa karibu na mshauri wa chama, na mzee mlezi wa chama.
  7. Kwa kadri inavyowezekana, shirikisha uongozi wa kanisa mipango ya chama mapema. Baada ya kuweka mipango/malengo na kupitishwa na wanachama, iwasilishe kwenye baraza la kanisa.
  8. Watie moyo wanachama kujiunga na kuhitimu Kozi ya Kiongozi Mwadventista na Kiongozi Mkuu.
  9. Kuratibu na kusimamia matukio ya shughuli za chama kama yalivyoainishwa katika miongozo ya chama.
  10. Kuandaa mipango na bajeti ya chama ya mwaka.
  11. Kuhudhuria baraza la kanisa kila linapoitishwa.
  12. Kuwatia moyo wanachama kushiriki mikutano mbalimbali ya chama katika ngazi mbalimbali za kanisa.
  13. Kuwatia moyo wanachama kujali na kushiriki ibada na programu mbalimbali katika kanisa mahalia.
  14. Kusimamia mikutano ya chama ya kila juma, na ya majuma maalumu.
  15. Soma na fahamu vyema mwongozo wa chama ili uifanye kazi kwa uhakika na ufanisi.
  16. Kuwa tayari kuwafikishia wanachama maelekezo toka ngazi za juu za kanisa.
  17. Kusimamia mapendekezo ya watendakazi wengine wa chama ambao hawachaguliwi na kamati ya uchaguzi/baraza la kanisa, na kupeleka kwenye baraza la kanisa kwa ukubali/ushauri.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayogawiwa na mkurugenzi wa chama.

 

b).  Miongoni mwa Majukumu ya KATIBU/MHAZINI WA CHAMA CHA MABALOZI:

  1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao na mikutano ya chama.
  2. Agawe na kupokea fomu za kujiunga na chama.
  3. Aandike na kutunza orodha ya wanachama.
  4. Atunze kumbukumbu ya mapendekezo/mipango yote ya chama.
  5. Kutunza orodha ya wanafunzi katika vitengo mbalimbali-mfano:wanaosoma Biblia kwa mwaka, n.k.
  6. Kutayarisha taarifa fupi kila robo inayoonesha shughuli za chama zilizofanyika.
  7. Kupokea fedha zote za chama na kuziwasilisha kwa mhazini wa kanisa ili kuzitunza. Fedha hizo zitotolewa kwa mhazini wa kanisa kwa hitaji la chama.
  8. Kutunza kumbukumbu sahihi ya fedha zilizopokelewa na zilizotumika.
  9. Kuagiza vifaa vya chama kwa wakati.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayopewa na mkurugenzi wa chama.

 

 

c).  Miongoni mwa Majukumu ya MDHAMINI WA CHAMA CHA MABALOZI:

  1. Aelewe malengo, makusudi, na mbinu za programu za chama.
  2. Ni mshauri na mwelekezaji wa viongozi na maofisa wengine wa chama.
  3. Atende kama kiongozi anayewajali vijana; kuelewa mahitaji yao ni muhimu sana ili kutoa ushauri unaofaa kwa wakati ufaao.

 

 

  1. C.     Chama cha Watafuta Njia (PF):

Chama cha Watafuta Njia ni programu iliyojengeka kikanisa ambayo hutoa nafasi ya kujenga roho ya ujasiri na uvumbuzi inayopatikana katika kila kijana mdogo.

Hii ni pamoja na shughuli zilizotayarishwa kwa makini katika kuishi nje, uvumbuzi wa viumbe, ufundi wa kazi za mikono / sanaa, kujifunza Biblia, miradi ya kushuhudia, matembezi mashambani, kuendesha baiskeli, na matukio ya ujasiri mengi ya kupendeza.

Chama hiki huhusisha vijna wa umri kutoka miaka 10 hadi 15.

 

a). Miongoni mwa Majukumu ya MKURUGENZI WA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA:

       1. Kuandaa mikutano ya kawaida na ya mafunzo ya wanachama.

        2. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama.

        3. Kupata kuelewa shughuli za chama kwa makanisa mengine (ya Waadventista wa Sabato)

          ili kupata mambo ya kutia moyo.

  1. Wape majukumu wengine kama inavyolazimu katika kutekeleza mipango ya chama.
  2. Fahamu majukumu ya kila ofisa wa chama na fanya uwezavyo kuhimiza mafanikio ya chama.
  3. Uwe na ushirikiano wa karibu na mshauri wa chama, na mzee mlezi wa chama.
  4. Kwa kadri inavyowezekana, shirikisha uongozi wa kanisa mipango ya chama mapema. Baada ya kuweka mipango/malengo na kupitishwa na wanachama, iwasilishe kwenye baraza la kanisa.
  5. Kuratibu na kusimamia program za chama kama zilivyoainishwa katika miongozo ya chama.
  6. Kuandaa mipango na bajeti ya chama ya mwaka.
  7. Kuhudhuria baraza la kanisa kila linapoitishwa.
  8. Kuwatia moyo wanachama kushiriki mikutano mbalimbali ya chama katika ngazi mbalimbali za kanisa.
  9. Kuwatia moyo kujali na kushiriki ibada na programu mbalimbali katika kanisa mahalia.
  10. Kusimamia mikutano ya chama ya kila juma, na ya majuma maalumu.
  11. Soma na fahamu vyema mwongozo wa chama ili uifanye kazi kwa uhakika na ufanisi.
  12. Kuwa tayari kuwafikishia wanachama maelekezo toka ngazi za juu za kanisa.
  13. Kusimamia mapendekezo ya watendakazi wengine wa chama ambao hawachaguliwi na kamati ya uchaguzi/baraza la kanisa, na kupeleka kwenye baraza la kanisa kwa ukubali/ushauri.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayogawiwa na mkurugenzi wa chama.

 

b). Miongoni mwa Majukumu ya KATIBU/MHAZINI WA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA:

 1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao na mikutano ya chama.

  1.  Agawe na kupokea fomu za kujiunga na chama.
  2. Aandike na kutunza orodha ya wanachama.
  3. Atunze kumbukumbu ya mapendekezo/mipango yote ya chama.
  4. Kutunza orodha ya wanafunzi katika vitengo mbalimbali-mfano:wanaosoma Biblia kwa mwaka, wanaosoma madarasa ya pini na tuzo mbalimbali, n.k.
  5. Kutayarisha taarifa fupi kila robo inayoonesha shughuli za chama zilizofanyika.
  6. Kupokea fedha zote za chama na kuziwasilisha kwa mhazini wa kanisa ili kuzitunza. Fedha hizo zitotolewa kwa mhazini wa kanisa kwa hitaji la chama.
  7. Kutunza kumbukumbu sahihi ya fedha zilizopokelewa na zilizotumika.
  8. Kuagiza vifaa vya chama kwa wakati.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayopewa na mkurugenzi wa chama.

 

          c). Miongoni mwa Majukumu ya MDHAMINI WA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA:

         1. Aelewe malengo, makusudi, na mbinu za programu za chama.

  1. Ni mshauri na mwelekezaji wa viongozi na maofisa wengine wa chama.
  2. Atende kama kiongozi anayewajali vijana; kuelewa mahitaji yao ni muhimu sana ili kutoa ushauri unaofaa kwa wakati ufaao.

 

 

 

  1. D.    Chama cha Wavumbuzi (AC):

Chama cha Wavumbuzi ni programu ambayo imejengwa kwa wazazi-kanisa ambayo huwapatia wazazi zana ya kuweza kutumika kwa watoto wao wenye umri wa miaka 6 hadi 9 na kimekusudia kuamsha udadisi wao unaochomoza kuelekea ulimwengu unaowazunguka.

Programu hii ni pamoja na shughuli zinazolenga umri-mahsusi na ambazo huwahusisha wote mzazi na mtoto katika maburudisho, sanaa rahisi, kufurahia uumbaji wa Mungu, na shughuli nyinginezo zinazovutia kwa umri wao.

 

a). Miongoni mwa Majukumu ya MKURUGENZI WA CHAMA CHA WAVUMBUZI:

        1. Kuandaa mikutano ya kawaida na ya mafunzo ya wanachama.

        2. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama.

        3. Kupata kuelewa shughuli za chama kwa makanisa mengine (ya Waadventista wa Sabato)

          ili kupata mambo ya kutia moyo.

  1. Wape majukumu wengine kama inavyolazimu katika kutekeleza mipango ya chama.
  2. Fahamu majukumu ya kila mtendakazi wa chama na fanya uwezavyo kuhimiza mafanikio ya chama.
  3. Uwe na ushirikiano wa karibu na mshauri wa chama, na mzee mlezi wa chama.
  4. Kwa kadri inavyowezekana, shirikisha uongozi wa kanisa mipango ya chama mapema. Baada ya kuweka mipango/malengo na kupitishwa na wanachama, iwasilishe kwenye baraza la kanisa.
  5. Watie moyo wanachama kujiunga na kuhitimu madarasa ya wavumbuzi.
  6. Kuandaa mipango na bajeti ya chama ya mwaka.
  7. Kuhudhuria baraza la kanisa kila linapoitishwa.
  8. Kuwatia moyo wanachama kushiriki mikutano mbalimbali ya chama katika ngazi mbalimbali za kanisa.
  9. Kuwatia moyo kujali na kushiriki ibada na programu mbalimbali katika kanisa mahalia.
  10. Kusimamia mikutano ya chama ya kila juma, na ya majuma maalumu.
  11. Soma na fahamu vyema mwongozo wa chama ili uifanye kazi kwa uhakika na ufanisi.
  12. Kuwa tayari kuwafikishia wanachama maelekezo toka ngazi za juu za kanisa.
  13. Kusimamia mapendekezo ya watendakazi wengine wa chama ambao hawachaguliwi na kamati ya uchaguzi/baraza la kanisa, na kupeleka kwenye baraza la kanisa kwa ukubali/ushauri.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayogawiwa na mkurugenzi wa chama.

 

b). Miongoni mwa Majukumu ya KATIBU/MHAZINI WA CHAMA CHA WAVUMBUZI:

         1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao na mikutano ya chama.

                       2.  Agawe na kupokea fomu za kujiunga na chama.

              3. Aandike na kutunza orodha ya wanachama.

  1. Atunze kumbukumbu ya mapendekezo/mipango yote ya chama.
  2. Kutunza orodha ya wanafunzi katika vitengo mbalimbali-mfano:wanaosoma Biblia kwa mwaka, wanaojifunza Kozi ya Kiongozi Mwadventista, wanaojifunza Kozi ya Kiongozi Mkuu, n.k.
  3. Kutayarisha taarifa fupi kila robo inayoonesha shughuli za chama zilizofanyika.
  4. Kupokea fedha zote za chama na kuziwasilisha kwa mhazini wa kanisa ili kuzitunza. Fedha hizo zitotolewa kwa mhazini wa kanisa kwa hitaji la chama.
  5. Kutunza kumbukumbu sahihi ya fedha zilizopokelewa na zilizotumika.
  6. Kuagiza vifaa vya chama kwa wakati.

 

Msaidizi: Atatekeleza majukumu yote atakayopewa na mkurugenzi wa chama.

 

c). Miongoni mwa Majukumu ya MDHAMINI WA CHAMA CHA WAVUMBUZI:

  1. Aelewe malengo, makusudi, na mbinu za programu za chama.
  2. Ni mshauri na mwelekezaji wa viongozi na maofisa wengine wa chama.
  3. Atende kama kiongozi anayewajali vijana; kuelewa mahitaji yao ni muhimu sana ili kutoa ushauri unaofaa kwa wakati ufaao.

 

                        IDARA YA MAJENGO

  A. Baadhi ya Majukumu ya Kiongozi wa Majengo:

  1. Atawajibika kwa shughuli zote zihusuzo jengo la kanisa, majengo ya kanisa na kiwanja cha kanisa
  2. Atafanya utafiti kujua hali ya jengo la kanisa na kufanya utaratibu wa kufanyika kwa ukarabati pale penye matatizo.
  3. Anapaswa kulifanya vizuri eneo la kanisa na kuhakikisha kuwa linatunzwa na kulindwa.
  4. Awe na faili lenye habari zote muhimu za eneo hilo; kama ramani ya jengo, ramani ya eneo, uthibitisho toka Field/Konferensi kwamba kanisa lina Hati Milki, n.k.
  5. Chini ya kamati ya majengo atahakikisha kuwa eneo linawekewa uzio na kuwa na mipaka inayoonekana.
  6. Chini ya kamati ya majengo atahakikisha kuwa eneo la kanisa linaendelezwa kwa kupanda miti, kujenga jengo kwa ajili ya watoto au huduma nyingine muhimu.
  7. Atatoa taarifa mara moja kwa robo kwenda Field/Konferensi.
  8. Atatoa taarifa ya majengo, mafanikio na matatizo kwa baraza la kanisa au kwa washiriki.
  9. Atawasilisha mahitaji ya majengo kwa baraza la kanisa kwa kadri ya mahitaji.
  10. Atasimamia na kufuatilia utekelezaji wa maazimio yote ya kamati ya majengo na baraza la kanisa yahusuyo majengo.
  11. Atatoa taarifa kwa uongozi wa kanisa/baraza la kanisa/mchungaji endapo kuna shida au tatizo lihusulo kiwanja au jengo la kanisa.
  12. Baada ya zamu yake atahakikisha kuwa faili la majengo na nyaraka zake anazikabidhi kwa kiongozi wa majengo mpya.

 

Zingatia: Maswala yote ya viwanja yatakayotakiwa huduma ya serikali yatashughulikiwa na mchungaji wa mtaa au mtu ye yote lakini kwa ruhusa ya mchungaji wa eneo husika.

 

  B. Kamati ya Majengo:                                                                                                                                              Kamati inaweza kuwa na wajumbe wafuatao:-

  • Mzee wa kanisa kama mwenyekiti.
  • Mkuu wa majengo kama katibu.
  • Mtunza hazina wa kanisa.
  • Mwenyekiti wa kamati ya uwakili na maendeleo.
  • Na wengineo wanaoonekana kuwa wanafaa.

 

C. Mambo mengine kwa ajili ya maeneo ya kanisa:

  1. Eneo liwe katika hali ya usafi na unadhifu.
  2. Jengo la kanisa liwe lenye hadhi na mvuto wa heshima katika muonekano wake.
  3. Vyoo safi vya kutosha-wanawake, wanaume, wahudumu. View na milango