MTAA WA TEGETA ni tovuti inayoendeshwa na mtaa wa Tegeta unaoundwa na makanisa matatu ya Tegeta, Tegeta Beach, na Boko uliopo katika jiji la Dar es Salaam. Tovuti hii itakuhabarisha yanayotokea katika mtaa huo katika kupeleka injili kwa watu wote na hivyo kuwatayarisha kuonana kwa shangwe na Bwana wao Yesu Kristo arudipo hivi karibuni. Tovuti hii itakuelimisha pia kwa mada za kiroho, kiafya, na kijamii zitakazokuwezesha kukabili changamoto za maisha yako kwa ufanisi mkubwa. Karibu ufuatane nasi.